Header Ads Widget

TANZIA: MFANYABIASHARA MT HUWEL AFARIKI DUNIA

 


MFANYABIASHARA MKUBWA MKOANI IRINGA  MANSOOR THABIT HUWEL AMEFARIKI NCHINI  INDIA MAZISHI YATAFANYIKA INDIA  

ALLAH AMSAMEHE NA AMTHIBITISHE KAULI THABIT.

Mchezaji maarufu wa Mbio za Magari nchini Ahmed Huwel (Kushoto) akiwa na babake Mzee Huwel Enzi za uhai wake.

Kwa taarifa za familia maziko yatafanyika kesho India, saa nane mchana ya kule, msiba upo nyumban Iringa kwa muda huo huku itakuwa saa sita patakuwa na kisomo kwa muda huo wa maziko Khallu innallilah waina Illahi rajiun
 

HAKIKA IRINGA TUMEFIWA 😭😭😭

Inalilahi wa inalilahi rajuun mbele yeye nyuma sisi Tangulia Mzee Mansour Thabit Huwel wengi hukusikia tu kuliko kukufahamu maarufu Kwa Jina la MT huwel marehem ni Moja Ya tajiri mkubwa.

Lakini Mzee wetu huyu amewekeza Sana mkoani Iringa Kwa nyanja ya usafiri wa malori,vituo vya mafuta viwanda vya Maji na tumbaku na kufanya Watu wengi wa Mkoa Wa Iringa kupata ajira na kuweza kumudu kuendesha Maisha bila shida kupitia Mzee wetu huyu.

Sifa nyingine ukipita nyumbani Kwake cku Ya Ijumaa Kama leo utakuta Watu wengi wenye uhitaji(omba omba)wamejaa mlangoni wakimsubiri awasaidie hii imenitafakalisha Sana anazikwa ljumaa na misaada alikuwa anatoa Ijumaa (Namuona Mungu kaamua kumchukua mja wake Kwa wakati Wake ya Mungu tumuachie Mungu)nje hayo Mzee wetu huyu alisaidia Sana nyanja ya Jamii Kwa mfano serikali na kwenye michezo.

Nimalize Kwa kusema mwanae Ahmed huwel " mkwawa" alitutoa ushamba akatuletea mbio za magari najua atarithi mazuri ya Baba Yake bila majivuno Wala kiburi.
Ni mm mchokozi


🛑karibu utangaze na Matukio Daima media ☎️0673791054/0747044508
Post a Comment

0 CommentsMAGAZETIBBC NEWS