Header Ads Widget

SIMBA SC KUMEKUCHA TRY AGAIN NA WENZAKE WAJIUZULU

 


BUNDI atua ndani ya klabu ya Simba SC klabu baada yawajumbe wa bodi ya wakurugenzi upande wa Mwekezaji Mohamed Dewji  kuanza kujiuzulu nafasi zao.


Taarifa zinasema kuwa MO amewapigia wajumbe wake wote akiwataka waandike barua za kujiuzulu kwa lengo la kuunda safu mpya ya uongozi kabla ya kuanza mchakato wa usajili mpya.


Kwa mujibu wa chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya Simba kimedokeza Matukio Daima media kuwa ni viongozi wote wa bodi ya Simba wametii wito wa kiongozi wao ambaye ndiye aliyewateua kwenye bodi hiyo.


"Hadi sasa ni wajumbe wote tayari wamejiuzulu kama mambo yataenda sawa kesho au keshokutwa Barbara Gonzalez atatangazwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi wa muda wa timu hiyo ili mambo yaende.


"Simu hizo amepiga kwa wajumbe wa upande wake pekee kwani ndio ambao anauwezo wa kufanya uamuzi huku kwa upande wa klabu viongozi waliopitishwa na wanachama kwenye mkutano mkuu wanaendelea na majukumu yao kama kawaida." kimesema chanzo hicho.


Wajumbe hao wa Bodi waliokuwa chini ya Mwenyekiti, Salum Abdallah Muhene 'Try Again' ni Dk. Raphael Chageni, Hamza Johari, Zulfikar Chandoo na Rashid Shangazi.


Hata hivyo, chanzo hicho kinasema baada ya kuingia mwenyekiti mpya timu hiyo itaanza harakati za usajili na kutafuta kocha mpya wa timu hiyo.

karibu utangaze na Matukio Daima media ☎️0673791054/0747044508
Post a Comment

0 CommentsMAGAZETIBBC NEWS