Header Ads Widget

TADB WANUFAISHA VIJANA WAFUGAJI NCHINI WANUFAIKE KIUCHUMI

 





Bank ya Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania TADB imedhamilia kuwakwamua wafugaji kiuchumi ambapo wametoa mikopo katika sekta ya ufugaji shilingi bilioni 25 zimetolewa katika mnyololo wa thamani wa Mifugo hasa katika unenepeshaji wa Mifugo na ng'ombe wa maziwa.


Akitoa taarifa katika ufunguzi wa Maonyesho Jumuhia ya Wafugaji kibiashara nchini TCCS  Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bank ya TADB Frank Nyabundege huko Ubena Chalinze mkoani Pwani ambapo Wafugaji kiboashara na Wadau wake wanaonyesha shughuli zao.


Amesema kwa kuanzia mradi wa kuwezesha vijana ikiwa ni kuunga mkono Nia ya Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan anayetaka kuona vijana Wafugaji wanawezeshwa bank hiyo imetenga shilingi milioni 279  kwaajili ya kukopesha vikundi vya vijana.


Amesema Bank hiyo huwasaidia vikundi vya vijana vyenye idadi ya vijana kuanza na vijana watano katika sekta ndogo ya maziwa na tumeanza katika mkoa wa Tanga kwakushirikiana na shirika la linaitwa solitalidad.


"Dhamira yetu ni kulenga vijana kujikwamua kiuchumi yaani kujiajili kupitia mradi huo ambapo vijana wanapewa mkopo kwa riba ya asilimia saba  n walie kwa miaka saba ambapo pia mkopo huu unakwenda kumuwezesha kijana kununua shamba lenye ukubwa wa ekari tano mpaka kumi"


Amefafanua kuwa pia mikopo hiyo huwasaidia vijana kujenga nyumba ya kuishi na kujenga banda bora kwa ajili ya  wa hao ng'ombe kufugia ng'ombe kumi na hao ng'ombe kumi wa maziwa, umwagiliaji katika shamba hilo la malisho na pia kupata vifaa kwa ajili ya kushiriki katika ufugaji.


Aidha Mkurugenzi huyo ameahidi kuendelea kufadhiri Maonyesho hayo ya wafugaji kiboashara kwa kusema "Sisi tutakuwa ndio wafadhiri wenu wakubwa kwa kadri mtakavyofanya maonyesho maana Rais wa Tanzania anawajali wananchi wake wote hasa wakulima na wafugaji, mwaka unaofata pia tutakuwa ndio wafadhili wa event hii"


Awali Mwenyekiti  wa Jumuiya ya Wafugaji wa Kisasa  Tanzania NCCS ,Naweed Mulla amemshukuru Mheshimiwa Rais  wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt .Samia Suluhu Hassan kutikana na serikali  kuwashika mkono  wafugaji wa kisasa.


Mulla amesema  kuwa maonesho haya yanalenga  kuwanyanyua  wananchi  na wafugaji wa kisasa pamoja na  kuwawekea  mazingira  sahihi huku amesema kuwa  kauli mbiu ya mwaka huu inasema  tufuge kibiashara  tuijenge kesho iliyo bora.


"Mhe.Rais amekua akitupa maneno ya  kututia moyo  pindi awapo katika majukwaa mbalimbali  jambo ambalo linazidi kutuje nga na kutukuza zaidi"amesema Naweed.


Mwenyekiti huyo wa NCCS Naweed amesema kuwa Mh.Rais amewapa bajeti mara mbili kwa kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi hivyo tunaahidi kutoa  ushirikiano  wa kutoa maoni  yetu  katika sekta hii ya ufugaji wa kisasa na tuna ahidi tutakuwa naye begakwabega katika kukuza uchumi wa nchi kupitia ufugaji wa kisasa.


Naibu Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Alexander Mnyeti akifungua Maonyesho hayo aliwapongeza Jumuhia ya Wafugaji kibiashara kwa kufanya Maonyesho hayo yanayoonyesha Uhalisia wa ufugaji wa kibiashara ambao utasaidia kuongea Soko la nyama ya Tanzania Kimataifa.


Tanzania  ni nchi ya pili kwa mifugo barani Afrika pia tuna ng'ombe  zaidi ya Mil.37.


Maonesho  hayo yamefunguliwa jana na Naibu Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Alexander Mnyeti  yafungwa kesho ambapo mgeni rasmi atakuwa Naibu Waziri Mkuu Biteko.

+++++++++

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI