Header Ads Widget

RC NJOMBE AAGIZA WANGING'OMBE KUFUNGA HARAKA HOJA 7 ZA CAG.



Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE


Mkuu wa mkoa wa Njombe Antony Mtaka amemuagiza mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya  ya Wanging'ombe Dokta Peter Nyanja kuhakikisha anafunga haraka Hoja saba za ukaguzi zilizobainika kuwa na mapungufu katika ukagizi wa Mdhibiti na mkaguzi mkuu wa  hesabu za serikali CAG.


Katika mkutano maalumu wa baraza la Madiwani wilayani Humo Mtaka amesema kwa kuwa kufungwa kwa hoja hizo kutaisaidia Halmashauri kupiga hatua kimaendeleo hivyo ni lazima zoezi hilo lifanyike kwa haraka.



Sanjari na hilo lakini pia Mtaka amewataka Wanasiasa wilayani Wanging'ombe kuacha tabia ya kuwekeana chuki na hila kwani haileti afya kwenye maendeleo ya Wananchi.



Awali mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Wanging'ombe Dokta Peter Nyanja amesema katika hoja hizo saba ambazo hazikufungwa zipo hoja zinazotokana na Ucheleweshwaji wa Fedha za miradi toka serikali kuu,Kukosekana kwa usawa katika utoaji mikopo ya asilimia 10 pamoja na baadhi ya watumishi kuwa na madeni zaidi ya uwezo wao.



Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Wanging'ombe Agnetha Mpangile amekiri kupokea maelekezo ya mkuu wa mkoa juu ya kutatua changamoto zao za kisiasa huku madiwani akiwemo Annaupendo Gombela wakiagiza kufungwa kwa hoja hizo na ripoti waipate katika mkutano wa Baraza la mwezi Oktoba.


Hata hivyo Katibu tawala mkoa wa Njombe Judica Omary amesema halmashauri hiyo imekuwa ya mfano katika utendaji wake kwani licha ya kupata hati safi lakini tayari wameshafikisha asilimia 100 katika makusanyo ya ndani.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI