Header Ads Widget

WATEJA 14 WA TANESCO MOROGORO WASITISHIWA HUDUMA KWA TUHUMA ZA UHUJUMU MIUNDO MBINU ..

Na Matukio Daima Media Morogoro

VIONGOZI na Wananchi katika wilaya za Kilosa,Mvomero na  Morogoro Manispaa wamelaani vitendo vya hujuma dhidi ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), baada ya wateja 14 kubainika wakitumia umeme kinyume cha sheria na kusitishiwa huduma hiyo.

Baadhi ya viongozi wa maeneo mbalimbali akiwemo Khafani Abdallah, Mwenyekiti wa Kijiji cha Milama kata ya Dakawa wilaya ya Mvomero, na Saidi Daudi, Mwenyekiti wa Mtaa wa White House kata ya Mafisa Manispaa ya Morogoro, wamepongeza hatua hiyo wakisema itawasaidia wananchi kuacha njia za panya na kulinda miundombinu ya umeme kwa manufaa ya wote.

Mhandisi Mkuu wa TANESCO Kaskazini Morogoro, Adam Abdula, amesema oparesheni iliyofanyika imelenga kulinda mali za umma na itakuwa endelevu ili kudhibiti upotevu wa mapato na kuimarisha huduma kwa wananchi.

Miongoni mwa waliokamatwa ni Salim Ally, mkazi wa Kijiji cha Madudu wilayani Kilosa na mfanyabiashara wa mashine za kusaga, ambaye alidaiwa kujiunganishia nyaya za umeme bila kufuata utaratibu rasmi wa TANESCO.

Mfanyabiashara huyo Alisema aliwaamini mafundi bila uhakiki na kujikuta miongoni mwa vipande  vilivyotumika kumuunganisha Umeme vilikuwa vya TANESCO, sambamba na kukiri kugundulika na mapungufu mengine kwenye uhamishwaji wa mita (meter transfer)

Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI