Na Hamida Ramadhan Matukio Daily App Dodoma
RAIS wa Tanzania Dkt, Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya miaka 69 Jumuiya ya wazazi tangu kuanzishwa kwake mwaka 1977.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dodoma Fadhil Rajabu Maganya Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi Taifa amesema maadhimisho ya wiki ya wazazi kitaifa itafanyika Mkoa wa Katavi Wilaya ya Mpanda kuanzia tarehe 13 hadi 15
Maganya ambaye pia ni mjumbe wa kamati kuu CCM Taifa amesema kwa mwaka 2024 Jumuiya Inaadhimisha miaka hiyo 69 ambapo baada ya maadhimisho hayo sherehe hizo zitafanyika katika ngazi mbalimbali za uongozi nchi nzima kunzia ngazi ya Tawi, kata, wilaya, na Mkoa .
Maganya amesema wanatarajia kufanya ufunguzi wa maadhimisho hayo Julai 8, mwaka huu katika Mkoa wa Katavi Wilaya ya Mlele kata ya Inyonga kwenye viwanja vya Shule ya msingi Inyonga.
" Katika wiki hiyo tutaitumia kwa kupanda miti zaidi ya 100,000 lengo likiwa ni kutunza mazingira, " Amesema Mwenyekiti huyo Maganya
Amesema Julai 10 kutakuwa na Baraza kuu la kawaida la Umoja wa Wazazi Tanzania,Julai 11, Julai Kongamano la maadili na Malezi,na Julai 12 itakuwa maalum kwa ajili ya michezo.
Katika hatua nyingine Maganya ameeleza kuwa kauli mbiu ya Sherehe hizo kwa mwaka 2024 ni Uchaguzi 2024/2025, Jumuiya ya Wazazi iko mstari wa mbele.
Katika Hatua nyingine Mwenyekiti huyo amempongeza Mkuu wa wilaya ya Ubungo Jijini Dar es salaam Hassan Bomboko na Mkuu wa mkoa Albet Chalamila kwa kusimamimia maadili.
Amesema Jumuiya ya wazazi ndio yaenyedhamana ya kusimamimia maadili, Elimu, malezi, mazingira na afya hivyo kumekuwepo na malalamiko kwa Mkuu wa Wilaya huyo Hassan Bomboko kwa Kushugulika za kinadada wanaouza miili yao yani Dada Poa huku wakitaka kulipwa fidia.
"Kwaniba ya Jumuiya tunatoa kauli ya kumuunga mkono na kumpongeza Mkuu wa wilaya ya Ubungo kwa kazi nziri anayoifanya na tunatoa wito kwa biongozi wengine kuendelea kufanya kazi kwa kusimamimia sheria, " Amesema
Na kuongeza " Haiwezekani Mambo ya hovyo ynafanyika Sisi tupo tunayaona na kuyasikia lakini tumekaa Kimya hivyo Jumuiya ya wazazi tutakuwa pamoja na serikali kwa hatua Toyota itakayochukuliwa kuhusiana na suala hili la biashara ya Dada Poa, " Amesema amesema maganya mjumbe wa kamati kuu CCM Taifa
Mwisho
0 Comments