Na Hamida Ramadhan Matukio Daima app Dodoma
WABUNGE wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wameshiriki bonanza la CRDB Bunge Grand Bonanza lillilofanyika katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma,Juni 22,2024.
Bonanza hilo limeongozwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Hemed Suleiman Abdulla pamoja na viongozi mbalimbali akiwemo Naibu Waziri mkuu na Waziri wa Nishati Dkt.Doto Biteko,Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Tulia Ackson.
Katika bonanza hilo michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu,mpira wa pete,kufukuza kuku ,kupokezana vijiti kula ,kunywa soda kukimbia na magunia mbio za riadha na michezo mingine.
Aidha dhumuni kuu la bonanza hilo ni kuwezesha ujenzi wa sekondari ya wavulana (Bunge Boys),kujenga afya pamoja na kuimarisha ushirikiano na taasisi mbalimbali.
Akiongea katika Bonaza hilomakamu wa pili wa Rais wa serikali ya mapinduzi Zanzibar Hemed Suleiman Abdulla amesema Bonaza hilo linalenga kuhakikisha afya za watanzania zinakuwa salama hali itakayoasaidia Serikali kuondokewa na mzigo makubwa wa maradhi yasioambukiza.
Amesema Bonanza hilo linakwenda kuhamaisha jamii kuwa na utaratibu wa kufanya mazoezi.
"Ninaimani baada ya bonanza hilo kwa wabunge sasa hata wananchi wenu mnao wawakilisha watakwenda kutambua umuhimu wakufanya mazoezi kwa afya zao, "Amesema
Kwa upande wake Spika wa Bunge Dkt Tulia Ackson amesema wamekuwa na mabonazo ya mara kwa mara na yote mabonaza hayo yamekuwa na maana Maalumu.
" Tumekuwa na mabonazo ya mara kwa mara lakini nia yetu ni tuache alama kwani kupitia mabonazo haya tumeweza kufanikisha kujenga shele ya Bunge wasichana na sasa tunajenga shule ya Bunge wavulana, " Amesema Dkt Tulia.
Mwisho








0 Comments