Na WILLIUM PAUL.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Taifa Komredi Mohammed Ali Kawaida (MCC) amewapongeza Wasomi wa Vyuo na Vyuo Vikuu Seneti ya UVCCM Mkoa wa Dar es Salaam wanaohitimu Elimu Yao ya Vyuo Vikuu tarehe 16 Juni 2024.
"Ndugu zangu niwapongeni sana kwa hatua hii mliyofikia leo hii mnahitimu Elimu zenu za Vyuo na Vyuo Vikuu, hatua hii ni kubwa mno kwani ndani ya Miaka 3-4 mmepitia mamb mengi sana ikiwepo Sup na kadhalika hivyo mnastahili sana Pongezi kwa hatua hii"
"Mmeshapata Elimu zenu sasa mnarudi mtaani, kule mtakuta watu wengi sana na wengi sio Kila aliyepo mtaani amesoma wengi Wana Elimu za kawaida tu na inawezekana wakawa wamekuzidini maarifa lakini nataka niwaambie mafanikio ya Maisha yako unayo wewe mwenyewe, nendeni mkashirikiane na Wananchi wenzenu Vyema"
"Nendeni mkazitumie taaluma zenu kusaidia jamii zenu zinazowazunguka, hata uwe na Uwezo kiasi gani, Kuna mambo usipoyazingatia unaweza usifanikiwe au usifike tunapotaka"
Mwisho Komredi Kawaida amewasili Vijana kuendelea kuwa wamoja na kutokuta tamaa kwani hata historia yake ya Uongozi tangu alipomaliza Elimu ya Vyuo na Vyuo Vikuu ni matokeo ya kutokukata tamaa.
0 Comments