Na WILLIUM PAUL.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Komredi Mohammed Ali Kawaida (MCC) amesisitiza Serikali kufungia Mtandao wa X ambao Zamani ulijulikana kama Twitter Ili kulinda utamaduni wa Taifa letu.
Ndugu Kawaida ameyasema hayo alipokua anahutubia wasomi wa Vyuo na Vyuo Vikuu UVCCM Mkoa wa Dar es Salaam tarehe 16 Juni 2024.
"Ndugu zangu Kuna mtandao unaitwa X, Mtandao huu Zamani ulikua unajulikana kama Twitter, hivi Karibuni mtandao huu umebadilisha sera zake za Uendeshaji na kuruhusu kupandishwa kwa maudhui ya kiutu Uzima (Maudhui ya Ngono)' nataka niwaambie kitendo cha mtandao huu kuruhusu maudhui haya ni kinyume na sheria zetu na Utamaduni wetu"
"Kuna watu baada ya Mimi kusema mtandao huu umefungwa wamekuja na hoja dhaifu za uhuru wa Vyombo vya Habari, ninyi hapa ni mashahidi RAIS Samia Suluhu Hassan alipoingia Madarakani ndiye aliyeruhusu uhuru wa Vyombo vya Habari na Kila mtu alipata nafasi ya kusema na wengine wanautumia Uhuru huo kumtukana lakini hakuna chombo Wala mtandao tuliosema ufungwe"
"Huu Mtandao tunasema ufungwe kutokana na Maudhui yake, lakini Cha Ajabu hakuna Kiongozi Wala taasisi yoyote ya Haki za Binadamu iliyojitokeza kutuunga Mkono kwani wana maslahi na Maudhui yanayoshapishwa kwenye Mtandao huu"
"Nataka niwaambie yaani ndio kwanza nimeanza ni ama Mmiliki wa huu mtandao abadilishe Sera zake maudhui yake ya Ngono yasionekane katika nchi yetu au Serikali kupitia TCRA kuuungia huu mtandao kulinda Sheria zetu na Utamaduni wetu" alisema Komredi Kawaida.
Mwisho..
0 Comments