Mgomo wa wafanyabiashara jijini Mbeya umeingia siku ya tatu leo alhamisi (Juni 27, 2024) ambapo wafanyabiashara bado wanaendeleza mgomo wa kutofungua maduka yao hadi pale Serikali itakapotatua kero zao ikiwemo utitiri wa kodi hivyo kuwa na mazingira magumu kwenye biashara zao.
Wakati mgomo huo ukiingia siku ya tatu jijini Mbeya na wengine siku ya nne, pia mikoa jirani ya Njombe (Makambako) na Songwe (Mlowo na Tunduma) bado migomo inaarifiwa kuendelea licha ya hapo jana (Juni 26, 2024) Waziri mkuu Mhe. Kassim Majaliwa kukutana na viongozi wa wafanyabiashara nchini huko jijini Dodoma.
0 Comments