Wakazi wa kijiji cha Ikombe kata ya Matema Wilayani Kyela Mkoani Mbeya wameiomba serikali iwatengenezee barabara kutokana na usafiri pekee wa majini wanaotumia katika ziwa nyasa na kwa sasa kuwa si wa uhakika kwani wakati mwingine wanashindwa kusafiri kutokana na dhoruba hivyo baadhi ya wagonjwa wanaohitaji huduma za dharula hupoteza maisha.
Tangu kuanzishwa kwa kijiji hicho mwaka 1976 hakijawahi kuwa na barabara hivyo wananchi hawa wamepenyeza ombi kwa serikali kupitia mbunge wao.
Mbunge wa jimbo la Kyela Ally Mlaghila Akatangaza neema kwa wananchi hawa wa kijiji cha Ikombe itakayosaidia kumaliza changamoto ya wanawake kujifungulia njiani wakielekea kutafuta huduma za kiafya.
0 Comments