Serikali ya Tanzania imekusudia kuanza kutumia michezo ya kubahatisha (kamari) kwa ajili ya kukusanya fedha zitakazotumika kulipia bima za watu wasiojiweza na makundi maalumu.
Hilo litawezekana baada ya kukusudia kuanza kutoza asilimia 10 kwenye thamani ya dau la kamari kwenye michezo ya kubahatisha.
Pia, imetangaza kutoza asilimia 10 katika kila ada ya matangazo ya biashara za michezo ya kubahatisha yanayotangazwa kupitia vituo vya televisheni, redio na uchapishaji.
Hayo yameelezwa leo na Waziri wa Fedha, Dk Mwigulu Nchemba wakati akisoma hotuba ya bajeti ya Serikali katika mwaka 2024/2025.
Dk Mwigulu amesema kupitia kuanzishwa kwa tozo hizo Serikali inatarajia kukusanya kiwango kikubwa cha fedha.
0 Comments