Header Ads Widget

USHURU WA MAJI KUPUNGUZWA

Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba akiwasilisha bajeti kuu ya Serikali ya mwaka wa Fedha 2024/2025 Bungeni Jijini Dodoma leo June 13,2024 amependekeza kupunguza ushuru wa bidhaa ya maji ya Tanzania yanayosindikwa kwenye chupa.

 “Napendekeza kupunguza ushuru wa bidhaa kutoka shilingi 63.80 kwa lita hadi shilingi 56 kwa lita ya maji ya kunywa yaliyosindikwa kwenye chupa yanayozalishwa Nchini” 

“Maji hayo yanatambulika kwa HS code 2201.10.00 na 2201.90.00, lengo la hatua hii ni kuchochea ukuaji wa Viwanda vidogo vinavyozalisha maji Nchini, kupunguza gharama kwa Walaji na kuchochea matumizi ya maji safi na salama, hatua hii inatarajia kupunguza mapato ya Serikali kwa kiasi cha shilingi milioni 474

 Dr. Mwigulu.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI