Header Ads Widget

KIJANA WA MIAKA 16 ALAWITI WATOTO WATATU KIHUWE NACHINGWEA



WANANCHI wa kijiji cha kihuwe kata ya Naipingo wamemlalamikia mkuu wa wilaya ya Nachingwea kwa kitendo cha kijana  anayelawiti wananchi kushindwa kuchukuliwa hatua za kisheria 

Wananchi hao walisema kuwa kijana anayejulikana kwa jina la Richard Kozimo A.k.A 69 amekuwa akiwalawiti watoto kwa kutumia nguvu bila kuwa na shaka yoyote ile ya kisheria 

Walisema kuwa wamemkamata mara kadhaa na kumfikisha kituo cha polisi lakini hukumu yake imekuwa ni viboko tu na kurudi kijijini na kuendelea na vitendo vya wizi na kulawiti watoto 


Akijibu kero hizo mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo alisema kuwa ameliagiza jeshi la Polisi kumfuatilia kijina huyo ili achukuliwe hatua za kisheria.

Moyo alisema kuwa serikali ya wilaya ya Nachingwea haitamvumilia mtu yoyote atakaye fanya vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa ujumla.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI