Header Ads Widget

DC SAME "RAIS AMEWEKEZA HANA DENI SAME SEKTA YA MAJI”

 


NA WILLIAM PAUL, SAME. 


MKUU wa Wilaya ya Same Kasilda Mgeni amewataka viongozi wa vyombo vya watumiaji maji kusimamia mapato na matumizi yanayokusanywa na vyombo hivyo ili kufanya miradi hiyo kuwa endelevu kwa matumizi ya vizazi vya sasa na vijavyo.  


Kasilda amezungumza hayo wakati akifungua mkutano wa wadau wa maji wilayani Same ambao umewakutanisha Wenyeviti na Watendaji wa vijiji Wilayani humo wenye lengo la kujadili na kushauriana namna ya usimamizi wa miradi ya maji inayotekelezwa na Serikali kupitia RUWASA.



“Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.  Samia Suluhu Hassan sisi wakazi wa Same hatuna deni naye kwenye sekta ya maji amewekeza fedha nyingi sana ambazo zinatekeleza miradi mbalimbali, ni jukumu letu sasa kama watendaji wa Serikali kuhakikisha kuwa hii miradi ambayo Rais amewekeza inasimamiwa vizuri” alisema Kasilda. 


Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Same, Yusto Mpande amewasisitiza viongozi hao kuwa wanajukumu la kuwaelimisha wananchi wajibu wa kuchangia huduma ya maji kiasi kidogo ili fedha zinazokusanywa ziweze kusaidia kuboresha miundombinu pamoja na uendeshaji wake.



Naye Meneja wa Wakala wa maji na usafi wa mazingira vijijini Wilaya ya Same RUWASA, Mhandisi Abdallah Gendaeka amesema kwa kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa Rasi Dkt. Samia wamepokea zaidi ya shilingi Bilioni 12.9 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maji vijijini.


Wilaya ya Same kunavyombo vitano vya watumiaji maji vilivyosajiliwa na kupewa jukumu la kukusanya bili za maji na kusimamia miradi ya maji ndani ya Wilaya ya Same kwa mujibu wa sharia.



Mwisho... 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI