Header Ads Widget

ZOEZI LA KUHAMA WANANCHI NGORONGORO LINAENDELEA KWA KUZINGATIA HAKI ZA BINADAMU

NA NAMNYAKI KIVUYO, ARUSHA.

Msemaji mkuu wa serikali Mobhare Matinyi amesema kuwa Tangu Juni 2022 hadi April 2024  jumla ya kaya 1,373 zenye jumla ya watu 8,364 zimeshahama kwa hiari katika eneo la mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro ambapo zoezi la kuhamasisha waliobaki linaendelea kwa kujali haki za binadamu pamoja na uhifadhi.

Matinyi aliyasema hayo leo Mei 26 wakati akiongea na waandishi wa habari ndani ya hifadhi hiyo kuhusu maendeleo ya mpango wa uhamaji wa hiari kutoka eneo la hifadhi kwenda kijiji cha Msomera na maeneo mengine ya nchi Kitwai na Saunyi.


Alisema kuwa takriban watu 100,000 wanatarajiwa kuhamia katika eneo hilo na katika eneo la Msomera  zinajengwa nyumba 2,500 ambapo nyumba 1,000 tayari na 737 zina wakazi, 263 zinasubiri kupokea watu huku 1,500 zikiwa katika hatua mbalimbali za ujenzi huku zikiwa zimeshaenda kaya 1,248 zenye watu 7,547 na meneo mengine wameshamia kaya 125 zenye watu 817 ikiwa ni pamoja na mifugo 36,457.

Alieleza kuwa katika kuendelea na zoezi hilo serikali kwa kushirikiana na NCAA wameweka mikakati ya uelimishaji na uhamasishaji  na uandikishaji katika kanda tano za Kaskazini, Kusuni, Magharibi, Mashariki na Kati mwa tarafa ya Ngorongoroi ili kuhakikisha kato zete 11 vinafikiwa kwa kupitia nyumba za ibada, minada, mikutano ya hadhara, kwa kukutana na baadhi ya viongozi wa kimila, watu maarufu ikiwa ni pamoja na wenyeviti wa vitongoji na vijiji.


“Lengo la mikakati yote hii ni kuhakikisha wananchi wanauelewa mpango huu wa uhamaji wa hiari unaojali haki za binadamu, umuhimu wa uhifadhi, sababu zake, faida na utekelezaji  ili kuondoa mashaka kwa wananchi wa Ngorongoro, nchi kwa ujumla na jumuiya za kimataifa,” Alieleza Matinyi.


“Uhamaji  unafanyika baada ya malipo ya fidia kukamilika, kuvunja makazi na kuchagua mali wanazotaka kuhama nazo, kusafiririshwa, ikiwa ni pamoja na kupewa fedha  za ziada ambapo kwa wanaohamia Msomeza wanapewa shilingi milioni 10 na wanaohamia maeneo mengine wanapewa shilingi milioni 15,” Alifafanua.

Aliendelea kusema kuwa  wananchi wanaohamia katika kijiji cha Msomera, na baade Kitwai na Saunyi  maandalizi huenda sambamba na hati ya nyumba ya vymba vitatu iliyo latika eneo la ukubwa wa hekari 2.5 na shamba binafsi la hekari tano  ikiwa ni pamoja na kupewa chakula kwa maana ya magunia mawili ya mahindi kwa kila baada ya miezi mitatu kwa kipindi cha miezi 18 wakati wakiendelea na maandalizi ya kuandaa mashamba yao kwaajili ya kilimo.

Aidha alifafanua kuwa kumekuwa na uvumi mbalimbali kuhusiana na kusitishwa kwa huduma kwa wananchi walio ndani ya hifadhi  wanaohama kunyimwa haki zao jambo ambalo sio lweli kwani  serikali bado imebeba jukumu la kuwahudumia wananchi ambao bado wanaishi ndani ya hifadhi mpaka watakapoamua kuhama lakini pia wananchi wote walihama kwa kufuata taratibu zote zilizowekwa wamelipwa stahiki zao zote kupitia mkuu wa kaya.

Pia akifafanua malalamiko ya baadhi wananchi waliokwa wakiishi katika pori tengefu la Msomera kwa kudai kunyang'anywa maeneo yao alisema kuwa wananchi hao hawajaondolewa japo kuwa walikuwa wavamizi badala yake wamepewa hekari mbili na nusu kwaajili ya makazi na shamba la hekari tano pamoja na hati miliki.

 Hata hivyo eneo la hifadhi ya Ngorongoro limeendelea kupokea idadi kubwa ya wageni kutoka maeneo mbalimbali Duniani ambapo kati ya mwezi Julai,2023 hadi Aprili, 2024 ilifikia 780,281 huku mapato yakiwa ni Bilioni 188,519,361,412 na kuvuka lengo la zaidi ya bilioni 155 ikiwa ni sehemu ya matunda ya Filamu ya Royal tour iliyofanya na Rais Samia Suluhu.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI