Header Ads Widget

WAZIRI NAPE: UHURU WA VYOMBO VYA HABARI UMEZIDI KUIMARIKA.

 


NA HAMIDA RAMADHAN, MATUKIO DAIMA APP DODOMA

WAZIRI wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amesema Uhuru wa vyombo vya habari nchini, umezidi kuimarika chini ya Serikali ya Awamu ya Sita kwa kuhakikisha kuwa vyombo vya habari vinakuwa huru kupokea na kutoa habari za matukio mbalimbali yanayojitokeza katika jamii.


Waziri huyo wa Habari amezungumza hayo leo Bungeni Jijini Dodoma wakati akiwasilisha Bajeti ya wizara kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025.


“Takwimu kutoka World Press Freedom lndex 2024 inayoratibiwa na Taasisi ya Reporters Without Boarders (RWB)(RSF) zimeonyesha kuwa Tanzania inaongoza kwa kuheshimu uhuru wa habari, Afrika Mashariki, na Kimataifa imeshika

nafasi ya 97 Mwaka 2024 toka nafasi ya 143 Mwaka 2023,” amesema Waziri Nape.


Aidha amesema, kuheshimu uhuru wa vyombo vya Habari, kumechangiwa na Serikali kuchukua hatua muhimu ikiwemo kufanya mabadiliko ya Sheria ya Huduma za Vyombo vya Habari ya Mwaka 2016, iliyoridhiwa na Bunge mwaka 2023.

ONGEZEKO LA VYOMBO VYA HABARI

Waziri Nape amesema vituo vya kurusha matangazo ya runinga vimeongezeka kutoka 65 mwaka 2023 na kufikia vituo 68 Aprili, 2024 sawa na ongezeko la asilimia 4.6.


Amesema Katika kipindi cha Mwaka wa Fedha 2023/2024, kumekuwa na ongezeko la vyombo vya habari lililochangiwa na Serikali kuendelea kuimarisha sekta ya hiyo nchini.



Amesema, kwa upande wa Cable Television, zimeongezeka kutoka 57 Aprili 2023 na kufikia 60 Aprili 2024, sawa na ongezeko la asilimia 5.3. 


Kwa upande wa vituo vya kurusha matangazo ya radio, vimeongezeka kutoka vituo 215 mwaka 2023 hadi kufikia vituo 231 Aprili 2024 sawa na ongezeko la asilimia 7.4, na magazeti yameongezeka kutoka 321 Aprili 2023 na kufikia 351 Aprili 2024, sawa na ongezeko la asilimia 9.3. 



Aidha, Waziri Nape amsema, Serikali imeendelea kuweka mazingira rafiki ya matumizi ya teknolojia za utangazaji hasa maudhui mtandaoni yaliyochangia pia kuongeza ajira kwa vijana waliojikita katika sekta hiyo inayoendelea kukua kwa kasi.


Hata hivyo katika tukio lingine Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati akizunguka kwenye mabanda ya wizara hiyo Bungeni jijini Dodoma amesema kuwa anamshukuru Rais Dkt, Samia Suluhu Hassan kwa kuhakikisha mifumo inakuwa bora nchini ambapo mafanikio hayo yameweza kuonekana kwa kila mtu kwani hata maofisini Mawasiliano kwa njia ya makaratasi hakuna tena.


Vile vile amesema amefurahishwa na Roboti Eunice kwa kuweza kuwasiliana na watu hivyo kuonyesha kwamba bajeti ya mwaka jana imefanya kazi lakini bajeti ya mwaka huu kufanya kazi na kwenda mbali zaidi kwani roboti huyo ataweza kuwepo sehemu mbalimbali kama hospitali na mahakamani ili kuweza kurahisisha utendaji kazi.


"Tunaimani hayo yote ni kutokana na jitihada za Rais wetu Samia tunaimani kuwa miaka mingine mitano ya uongozi wake ataweza kufanya mengi na makubwa zaidi kwani hivi sasa wananchi wanaweza kupata huduma hata wakiwa nyumbani pamoja na kufungua milango ya ajira kwa vijana wabunifu" Ameongeza ,Waziri Mkuu. 








Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI