Header Ads Widget

BENKI YA CRDB YATOA PIKIPIKI 20 KWA JESHI LA POLISI ARUSHA





Na,Jusline Marco:Arusha

Mkuu wa Arusha Paul Makonda amesema suala la ulinzi na usalama katika jamii linahitaji uwepo wa nyenzo muhimu katika jeshi la polisi ambapo amewataka wadau mbalimbali wa maendeleo kuunga mkono juhudi hizo.

Makonda ameyasema hayo wakati akikabidhiwa pikipiki 20 zenye thamani ya shilingi milioni 50 zilizotolewa na Benki ya CRDB kwa ajili ya kuimarisha ulinzi na usalama wa Mkoa wa Arusha ikiwa ni sehemu ya faida yake na kurudisha kwa jamii.


Aidha amesema anatambua kiwa usalama ni kivutio kimoja wapo katika kuvutia utalii ndani ya jiji la Arusha hivyo ameishukuru taasisi hiyo ya fedha kwa kuunga mkono juhudi hizo na kuufanya Mkoa wa Arusha kuwa Mkoa wenye amani na utuĺivu.

Akikabidhi vitendea kazi hivyo Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Abdulmajid Nsekela hatua hiyo ni uungaji mkono juhudi za mkoa wa Arusha na Serikali kwa ujumla katika kuhakikisha jeshi la polisi linakuwa na nyenzo za kisasa za kuleta tija ambapo kila mwaka benkj hiyo imekuwa ikitenga asilimia moja ya faida kurudisha kwa jamii.

Naye Kamanda wa polisi Mkoa wa Arusha Justin Masejo ameahidi kuimarisha ulinzi na usalama pamoja na kutumia vyema nyenzo hizo katika lengo lililokusudiwa.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI