WATAALAMU wa sekta ya Sukari na Miwa wamesema upatikanaji wa mbegu za miwa zenye kiwango kikubwa kwa ajili ya uzalishaji sukari zimetajwa kuwa ni changamoto inayoathiri ukuaji wa sekta hiyo licha ya jitihada zinazochukuliwa na Serikali kukabiliana na changamoto mbalimbali za Sekta ya Sukari.
Hayo yameelezwa mjini Morogoro na Katibu Mtendaji waJumuiya ya Chama cha Wataalamu wa Miwa na Sukari Tanzaniia, TSSCT, Bwana Federick Charles, wakati wa k ongamano la 10 lililoandaliwa na chama hicho likihusisha wataalamu mbalimbali wa wakiwemo kutoka viwanda vyote vya sukari vya Kilombero, Mtibwa, Mkulazi Holding company, Bagamoyo,Kagera na TPC pamoja na wataalamu kutoka taasisi zinazohusika na Sekta ya sukari
Akasema changamoto hiyo ya mbegu imewafanya wamiliki wa viwanda kuendelea kuagiza asilimia 90 ya mbegu kutoka nje ya nchi ikiwemo Malawi, Mauritius, Afrika ya Kusini na sehemu nyingine duniani.
Katibu Mtendaji huyo wa TSSCT akataja changamoto nyingine kuwa ni ya ukosefu wa mashine mbalimbali za viwandani ambazo nyingi zimekuwa zikiagizwa nje ya nchi na kusababisha gharama kubwa za uendeshaji na gharama kubwa ya sukari pamoja na ukosefu wa maabara ya kufanya uzalishaji wa mbegu za miwa.
Akawashauri wadau wa sekta ya sukari wa ndani na nje ya nchi kuona fursa ya kuwekeza vifaa vya kisasa vinavyohusiana na Sekta ya Sukari ili kujiongezea kipato lakini pia kurahisisha upatikanaji hapa nchini.
Frederick hata hivyo akaipongeza Serikali kufanya jitihada mbalimbali kuboresha sekta ya sukari ikiwemo kwa kudhibiti mfumuko wa bei na kuendelea kuwazalisha wataalamu wengi zaidi wa sekta hiyo.
Awali Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Adam Malima akifungua kongamano hilo aliwashauri wataalamu hao kujipanga kukabiliana na changamoto zilizopo sambamba na kutumia tafiti wanazofanya kuondoa changamoto zilizopo.
Akasema pia ni vyema wakiangalia namna ya kuwezesha ukuaji wa kilimo cha miwa hasa wakati huu ambao kinakabiliwa na changamoto ya mabadiliko ya Tabia nchi ambayo yameendelea kuathiri ukuaji wa sekta ya Sukari kutokana na Mashamba kujaa maji
Mkuu huyo wa Mkoa akawataka wataalamu hao kuwa wabunifu na kutumia teknolojia za kisasa ili kufanikisha malengo ya Taifa ya kuiinua Sekta hiyo.
Akimwakilisha Mkurugenzi mkuu wa bodi ya Sukari Tanzania,Bwana George Gowelle alisema hatua mbalimbali zimeendelea jym kuchukuliwa na Serikali kukabiliana na changamoto za sekta ya sukari.
Akasema Wizara ya Kilimo na taasisi ya Utafiti TARI Kibaha wameanza kuzalisha na kuzifanyia majaribio mbegu za Miwa.
"Kwa sasa kuna mbegu ambazo tayari zimeandaliwa kwa majaribio ikiwa ni pamoja na Tariska 121-122 ambazo tayari zimeanza kupandwa kwa majaribio katika maeneo mbalimbali"Alisema mwakilishi huyo wa bodi ya Sukari
Akataja miradi mingine mikubwa ni wa mbegu za Miwa utakaoanzishwa wilayaji Kilombero Mkoani Morogoro kwa kushirikisha Wizara ya kilimo, Bodi ya sukari, TARI Kibaha na wakulima wa bonde la Kilombero ambapo kitaanzishwa kitalu cha mbegu cha hekta 400 kwaajili ya kuzalisha mbegu ili kukidhi changamoto zilizopo.
Vitalu vingine vya mbegu za Miwa akasema vitaanzishwa katika kiwanda cha sukari Mtibwa kwaajili ya wakulima wadogo pamoja na kingine kitakachokuwa mkoani Manyara.
Mwisho.
0 Comments