Header Ads Widget

MIRADI 13 IMEZINDULIWA NA KUWEKWA MAWE YA MSINGI NA MWENGE WA UHURU WA 2024 MKURANGA




Na Scolastica Msewa, Mkuranga

Miradi 13 imezinduliwa na kuwekwa mawe ya msingi na Mwenge wa Uhuru wilayani Mkuranga yenye thamani ya shilingi zaidi ya bilioni 10.2 na kukimbizwa katika kilomita 85 za Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani.


Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Hadija Nassir Ally akitoa taarifa wakati wa kupokea Mwenge wa Uhuru wa mwaka 2024 huko Kipala mpakani katika Kata ya Mwandege wilayani Mkuranga ukiwa unatokea wilaya ya Kisarawe.


Alisema Mwenge huo wa Uhuru utaweka mawe ya msingi miradi 13 ya sekta ya afya, elimu, maji na bustani ya Miche ya misitu, shughuli za ujasiriamali wa vijana, uzinduzi wa darasa la utoaji wa elimu ya mapambano kupingwa na kuzuia vitendo vya rushwa TAKUKURU.


Kiongozi wa Wakimbiza Mwenge wa Uhuru kitaifa wa Mwaka 2024 Godfrey Mzava amepongeza uongozi wa Wilaya ya Mkuranga kwa usimamizi mzuri wa miradi ya maendeleo sambamba na umakini wa usimamizi wa fedha zinazoletwa wilayani humo.


Aidha alitoa pole kwa Wananchi walioathirika na mafuriko katika Wilaya hiyo ya Mkuranga na kuwataka kuendelea kuchukua tafadhali kwa kusikiliza maagizo ya serikali kwa kuhama katika maeneo hatarishi.


Waziri wa Mifugo na Uvuvi na Mbunge wa jimbo la Mkuranga Abdallah Ulega alipopewa nafasi ya kuzungumza kwaniaba ya Wananchi wa Wilaya ya Mkuranga alianza kwa kumshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa fedha za miradi ya maendeleo zinazoletwa wilayani humo.



Alisema kupitia Mwenge huo wa Uhuru miradi ya thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 10 imekaguliwa ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM kwamba umeweka jiwe la msingi na kukagua miradi hiyo ya maendeleo hasa mradi mkubwa wa maji ambayo kwa miaka mingi ilikuwa ahadi lakini Sasa imekamilika.


Alifafanua kuwa mradi huo utakuwa na uwezo wa kusambaza maji katika vijiji vya Kata nzima ya Kimanzichana itakuwa na uhakika wa kupata maji safi na salama.


"Sambamba na hilo Mwenge wa Uhuru umefingia maabara za kisasa za Sayansi ambazo zitakwenda kutengeneza madaktari, mainjinia, wabobezi wa fani mbalimbali nchini katika Wilaya hiyo jambo ambalo lilikuwa ni hitaji la Wananchi wa Kimanzichana kwa muda mrefu kwani watoto walisafiri umbali mrefu kufuata shule"

++++++

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS