Wanafunzi wa chuo cha ufundi Kigoma (KTC) wakiwa kwenye uzinduzi wa mradi wa Binti unatekelezwa na Shirika la AFRICRAFT
Na Fadhili Abdallah,Kigoma
WANAFUNZI kutoka vyuo vya kati mkoani Kigoma wameiomba serikali na wadau kuweka utaratibu rahisi utakaowezesha wanafunzi wa kike kupata taulo za kike kwa wepesi na kuweza kujistiri wanapopatwa na hedhi wakiwa vyuoni.
Wanafunzi hao wamesema hayo mjini Kigoma wakati wa uzinduzi wa mradi wa binti unaotekelezwa na Shirika lisilo la kiserikali la Africraft mradi unaoelenga kutoa elimu ya hedhi salama na ugawaji wa taulo za kike zinazoweza kufuliwa na kuvaliwa tena
Mmoja wa wanafunzi hao, Dercasia Petro Mwanafunzi wa chou cha ufundi Kigoma (KTC) alisema kuwa bado changamoto ya upatikaji wa taulo na kutokuwepo kwa vyumba vya kutumia kubadilishia taulo au kujistiri hivyo ameiomba serikali na wadau kuhimiza kuwezesha vyumba hivyo na taulo zipatikane kwa urahisi vyuoni.
Naye Ruth Razalo Mwanafunzi wa mwaka wa tatu anayesoma uuguzi katika chou cha ufundi Kigoma alisema kuwa Pamoja na changamoto ya ukosefu wa vyumba na upatikanaji wa taulo za kike ametaka pia mabinti kupata elimu ya kukabiliana na hedhi salama ili zisivuruge mipango yao ya masomo huku akitaka wadau na serikali kurahisisha upatikanaji wa taulo za kike.
Awali akizungumza kwenye uzinduzi huo Meneja mradi wa binti unaotekelezwa na Shirika lisilo la kiserikali la Africraft, Aneth Kivuyo alisema kuwa mabinti 12,000 wanatarajia kunufaika na elimu ya hedhi salama, afya ya uzazi na ugawaji wa taulo za kike kukabiliana na changamoto ya upatikanaji wa taulo hizo kwa wanafunzi.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika lisilo la kiserikali la Africraft, Kelvin Nicholous alisema kuwa kwa awamu hii wamelenga vyuo vya ufundi vya kati kutokana na pia kuwepo na mahitaji lakini pia wamelenga kundi hilo ili wanafunzi hao waweze kupewa elimu ya utengenezaji wa taulo hizo za kike na kusambaza kwa wanafunzi wenzao wa vyuo, shule za msingi na sekondari.
Dk.Albert Mwesigwa (katikati) Kaimu Mganga Mkuu wa mkoa Kigoma akikata utepe kuzindua mradi wa Binti unaotekelezwa na Shirika lisilo la kiserikali la AfricraftAneth Kiyao Meneja wa mradi wa Binti kutoka Shirika la AFRICRAFT akitoa taarifa ya mradi wakati wa uzinduzi wa mradi huo.
0 Comments