Na Mwandishi wetu Matukiodaimaapp
Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania –Tari Kituo cha Naliendele Dkt Furtunus Kapinga amewataka wakulima wa zao la ufuta kuzingatia taratibu zote kuanzia shambani hadi sokoni ili kuuza ufuta msafi wenye viwango sokoni.
Akizungumza wanachuo wa chuo cha kilimo Mtwara Naliendele MATI amesema kuwa ubora wa ufuta ndio utaweza kupandisha hadhi ya ufuta wetu sokoni ambapo mkulima anapaswa kuzingatia ushauri anaopewa.
Amesema kuwa ili uone kama ufuta uko tayari unapaswa kuangalia vitumba ambavyo huonekana kupasuka juu hivyo wakati wa kuvuna mwingi hupukutikia shambani.
“Wakati mwingine soko linakuwa zuri mkulima akawahi kuvuna na wakati mwingine anaweza kuchelewa akapoteza ufuta mwingi shambani hii inaweza kupelekea mkulima kupeleka ufuta sokoni ukiwa hauna ubora”
“Tunatoa pia mafunzo kwa wakulima wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali vinavyotoa elimu ya kilimo lakini pia hata chuo jirani cha MATI Mtwara pia wamekuwa wakifika hapa na kujifunza kuona tuanyofanya ya kiutafiti na kuoanisha na yale wanayosoma ili wanapotoka hapa waende kuwasaidia wakulima”
“Kwenye zao la ufuta tunaangalia ubora wa ufuta kuanzia shambani hadi sokoni na kumshauri mkulima afanye nini ili ufuta wake uweze kupata bei nzuri sokoni ambapo unaweza kukosa soko kwakutozingatia mambo ya msingi baada kuvuna ama kabla” amesema Dr Kapinga
Nae Mratibu wa programu ya ufuta kitaifa kutoka taasisi ya utafiti wa kilimo Tanzania tari kituo cha naliendele Joseph Nzunda amesema kuwa kuongeza uzalishaji wa ufuta unahitaji nguvu kubwa kama nchi ili kuongeza uzashaji wa zao hili.
“Hili zao linaweza kutupatia fedha za kigeni ndio maana tunahimiza kuongeza nguvu za uzalishaji zaidi kwakufanya tatifi mbalimbali ambazo zitaongeza zaidi uzalishaji ambapo tunakuja na mbegu bora yenye uwezo wa kukomaa ndani ya siku 80 kwenye mikoa yenye mvua wanaweza kulima mara mbili kwa mwaka” amesema Nzunda
“Yaani debe moja unapata 100,000 hii ni kama atm kwa mkulima anaweza kuuza wakati wowote na akapata pesa kutokana na faida kubwa iliyopo kwenye zao hilo hapa sasa tunapaswa tung’ang’anie kwenye ubora usishuke”
“Ni vema wakulima watimie mbegu bora zinazokubalika sokoni kwakufuata ushauri wa watalaam aapande kwa wakati apalilie kwa wakati atumie viwatilifu ambavyo ameshauriwa na watalaamu” amesema
Kwa upande wake Mtafiti wa Zao Ufuta kutoka Tari Kituo cha Naliendele Athanas Minja amesema kuwa wamefanikiwa kugundua mbegu zinazofanya vizuri sokoni zenye tija kubwa.
“Sokoni ufuta mweupe ndio una soko ambapo tunazo mbegu tayari ikiwemo lindi2002 ambayo inakomaa kwa siku 110 ina mavuno mengi lakini pia inafanya vizuri katika maeneo mengi ya nchi”
“Mkulima anapaswa ajue kuwa majani yakibadilika rangi kutoka kijani kwenda njano na yakaanza kupukutika aanze maandalizi ya kuvuna ambapo atatengeneza chanja na kuuweka ufuta huo ili ukauke wakati akifnaya maandalizi ya kuu”
“Upo umuhimu mkubwa kwa mkulima kujua namna bora ya kutunza ufuta baada ya kuutoa shambani ndio maana tunatoa elimu kwa wanfuzni ili wajue namna sahihi ya kulinda ubora wa zao hili” amesema Minja







0 Comments