Header Ads Widget

MRADI WA BBT KUANZIA NJOMBE KWA NGAZI ZA HALMASHAURI NCHINI

 




Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE

Wizara ya Kilimo kupitia mradi wa jenga kesho iliyo bora BBT imelazimika kuanzisha mradi huo kila Halmashauri nchini ili kuwasaidia vijana katika nyanja za kilimo na ujasiriamali mwingine.


Kwa hatua ya awali timu ya wataalamu toka wizara ya kilimo wakiongozwa na mratibu wa BBT  Vumilia Zinkankuba wamefika katika wilaya ya Njombe kushuhudia mpango wa mkuu wa wilaya ya Njombe aliyeanzisha programu ya Fursa kwa vijana na kuzulu kwenye Amcos ya Kilimo ya Isowelu Mtwango.


Vumilia na Msafara wake baada ya kufika katika shamba la Viazi Mviringo huko Mtwango amesema Mpango wa wilaya ya Njombe umewavutia na kuwalazimu BBT kuanzia Njombe kwa ngazi za Halmashauri ambako tayari kumeonesha mwanga na hivyo watakuwa bega kwa bega kuendeleza programu hiyo.


Awali mkuu wa wilaya ya Njombe Kissa Kasongwa amesema Kuna vijana zaidi ya 600 toka maeneo mbalimbali ambao wanatamani kufanya shughuli mbalimbali ili kukabiliana na changamoto ya uchumi na upungufu wa ajira nchini.


Mwenyekiti wa Isowelu Amcos  Bwana   Elia Mhonjwa amesema utaratibu wa kuwakopesha pembejeo wanachama wao umesaidia mkulima kupata gunia 80 hadi 200  za viazi kwenye shamba la ekari moja.


Baadhi ya Vijana hao  wamekiri kuwa na shauku kubwa ya kupata fursa hizo ambazo wanaamini zitawakwamua na changamoto za misuko suko ya maisha huku Baadhi ya wakulima na wafanyakazi wa mashambani kwenye kilimo cha viazi mviringo huko Mtwango wamesema wamekuwa wakinufaika na Kilimo hicho kupitia Isowelu Amcos kwani hivi sasa wameboresha maisha yao.


Viongozi wa Mradi wa Jenga Kesho iliyo bora BBT chini ya Wizara ya Kilimo wakiongozwa na mkuu wa wilaya ya Njombe Mhe.Kissa Kasongwa akiwa na zaidi ya vijana 200 wametembelea Katika kijiji cha Lunguya kata ya Mtwango kushuhudia kilimo cha viazi mviringo kinacholimwa na wanachama wa Amcos ya Isowelu

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI