Header Ads Widget

WAFANYAKAZI WAPONGEZA RAISI SAMIA ANAVYOSHUGHULIKIA KERO ZA0

Thobias Andengenye Mkuu wa mkoa Kigoma



Mratibu wa Shirikisho la vyama vya wafanyakazi (TUCTA) mkoa Kigoma Jumanne Magulu

Na Fadhili Abdallah,Kigoma


Wafanyakazi mkoani Kigoma wameipongeza serikali ya Raisi Samia Suluhu Hassan kwa kufanyia kazi kero na changamoto za wafanyakazi hali iliyosababisha kulipwa kwa stahiki nyingi za wafanyakazi.


Mratibu wa Shirikisho la vyama  vya wafanyakazi (TUCTA) mkoa Kigoma, Jumanne Magulu alisema hayo  akisoma risala kwa niaba ya vyama vya wafanyakazi wa mkoa Kigoma kwenye maadhimisho ya siku ya wafanyakazi yaliyofanyika kimkoa wilayani Kasulu.


Magulu kwa niaba ya wafanyakazi  ametoa pongezi kwa raisi Samia kwa upandishaji wa madaraja kwa watumishi wa umma, kupunguza muda wa upandishaji madaraja na kuondolewa kwa tozo ya asilimia sita ya mikopo kwa waliokuwa wanafunzi wa elimu ya juu.

Pamoja na hilo alisema kuwa bado wamekuwa na changamoto nyingi katika upatikanaji wa stahiki zao za madai mbalimbali ikiwemo nyongeza za malipo ya wastaafu wa muda mrefu ambao wamekua wakilipwa mafao kidogo ambayo hayaendani na hali halisi ya Maisha ya sasa Sambamba na kutaka kurekebishwa kwa kikokotoo cha mafao kilichopo sasa kirudishwe kile cha awali.

Akizungymzia kwenye maadhimisho hayo Mkuu wa mkoa Kigoma Thobias Andengenye alisema kuwa serikali ya awamu ya sita imefanya maboresho makubwa ya stahiki za wafanyakazi ikiwa ni kuondoa kero na changamoto mbalimbali zilizokuwa zikiwakabili kupitia sera na sheria mbalimbali.

  pomkja na hivyo Mkuu huyo wa mkoa ametaka maadhimisho ya siku ya wafanyakazi (MEI MOSI) yatumike kushughulikia changamoto za wafanyakazi na kumkomboa kikamilifu mfanyakazi katika nyana zote za kazi ilia pate stahiki zake zote bila kupunjwa

 hata hivyo  Mkuu huyo wa mkoa alisema kuwa yapo mambo ambayo waajiri kwa nafasi yao wanapaswa kushughulikia na kutoa wito waajiri kutimiza wajibu wao kwa kushughulikia stahiki za wafanyakazia na kuondoa changamoto zinazojitokeza.

 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI