Header Ads Widget

UNHCR YATOA MSIMAMO WAKE KWA WAKIMBIZI WA BURUNDI

 

Mkurugenzi wa idara ya wakimbizi ya wizara ya mambo ya ndani ya nchi Sudi Mwakibasi akionyesha Kipeperushi kilichotayarishwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi (UNHCR) kwa mashauriano na serikali ya Burundi na Tanzania kinachotoa maelezo na kuhamasisha wakimbizi wa Burundi kujiandikisha na kurejea nchini kwao kwa hiari.

 


Na Fadhili Abdallah,Kigoma

SHIRIKA la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi (UNHCR) limesema kuwa  wakimbizi wa Burundi wanaohifadhiwa kwenye makambi ya Nyarugusu na Nduta mkoani Kigoma wanapaswa kurudi nchini kwao sasa na kwamba huo ndiyo msimamo wa shirika hilo kwa sasa.

Mkuu wa Ofisi ya UNHCR wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma, Henock Ochala  akizungumza kwenye kambi ya Nduta wilayani Kibondo wakatk wa ziara ya  Mkurugenzi wa idara ya Wakimbizi ya wizara ya mambo ya ndani ya Tanzania, Sudi Mwakibasi aliyekuwa akifanya ziara kwenye kambi hiyo alisema kuwa hakuna uamuzi mbadala kwa wakimbizi wa Burundi zaidi ya kurudi nchini kwao.


Mkuu wa ofisi ya Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi (UNHCR) wilaya ya Kibondo Henock Ochala alisemaa hayo akizungumza mbele ya Mkurugenzi wa idara ya Wakimbizi ya wizara ya mambo ya ndani ya Tanzania, Sudi Mwakibasi aliyekuwa akifanya ziara kwenye kambi ya Nduta kupeleka taarifa kwa wakimbizi hao maazimio ya pande tatu ya kufungwa kwa kambi za wakimbizi wa Burundi ifikapo Desemba 31 mwaka huu.

Ochala alisema kuwa maazimio ya pande tatu ya kufungwa kwa kambi za wakimbizi wa Burundi ifikapo Desemba 31 mwaka huu yanaendeleza kutekelezwa na kwamba UNHCR inatekeleza jukumu lake kuhakikisha wakimbizi hao wanarejea.

Alisema kuwa shirika hilo limeandaa vipeperushi kwa lugha ya Kirundi, kifaransa, Kingereza na vile vya lugha ya Kiswahili vipo kwenye mchakato, alisema kuwa tathmini inathibitisha kwamba Burundi kwa sasa kuna amani na hivyo wakimbizi hao hawana sababu ya kuendelea kuishi makambini kwa hadhi ya ukimbizi bali kurudi nchini kwao.

 


Akizungumza katika mkutano na wakimbizi kwenye kambi ya Nduta wilayani Kibondo mkoani Kigoma Mkurugenzi wa idara ya wakimbizi ya wizara ya mambo ya ndani ya Tanzania,Sudi Mwakibisi alisema kuwa kwa sasa na kwa unyenyekevu wanatoa wito kwa wakimbizi wa Burundi kujiandikisha kwa hiari ili waweze kusafirishwa na kurudishwa nchi kwao wakipewa pia misaada mbalimbali ambayo itawasaidia wakati wa urejeshaji huo na kwamba muda uliowekwa ukiisha hata misaada hiyo haitakuwepo.

Kwa upande wake Mratibu wa idara ya wakimbizi kanda ya magharibi, John Mwita alisema kuwa hadi sasa jumla ya wakimbizi wa Burundi 168,000 wamerushwa nchini kwao tangu mwaka 2017 hivyo inashangaza kuona baadhi ya watu wako kambini hapo kama wakimbizi wakati wenzao wapo nchini mwao wakiendelea na shughuli nyingine za Maisha yao ya kila siku.

 

Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI