Header Ads Widget

RUNALI WATUMIA ZAIDI YA MILIONI 38 KUBORESHA ELIMU WILAYA TATU ZA MKOA WA LINDI

 

CHAMA kikuu cha ushirika mkoa wa Lindi (RUNALI) kinachohudumia wilaya ya Nachingwea, Ruangwa na Liwale kimetumia zaidi ya millioni 38 kuboresha sekta ya elimu katika wilaya hizo

Akizungumza na mwandishi wa habari, mwenyekiti wa RUNALI Odas Mpunga alisema kuwa katika msimu wa mavuno wa mwaka 2023/2024 wametoa zaidi ya shilingi millioni 38 kwa ajili kuboresha miundo mbinu ya elimu msingi na sekondari katika wilaya tatu za mkoa wa Lindi.


Mpunga alisema kuwa kila mwaka chama cha ushirika RUNALI kimekuwa kinarudisha kwa jamii sehemu ya faida wanayoipata baada ya mauzo ya mazao kwa msimu husika.


Alisema kuwa wakulima wanaotumia kuuza mazao kupitia chama cha RUNALI wamekuwa wanapata faida kulinga na thamani ya mazao yao ambayo yanakuwa yameongezewa thamani na chama hicho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI