Header Ads Widget

RC AAHIDI KUTOA MIKATE NA SIAGI KWA WATUMISHI WA UMMA

 


MKUU wa Mkoa wa Kusini Unguja Ayoub Mohammed Mahmoud ameahidi kuanza kutoa Mikate na siagi kwa ajili ya chakula cha Asubuhi kwa Watumishi wote ndani ya ofisi ya mkoa kusini Unguja ili kuongeza ufanisi wa kazi katika ofisi hiyo


Ahadi hiyo ameitoa leo Mei 04,2024 Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja wakati akizungumza katika Mkutano na Watumishi wa Umma ambapo amesema kuanzia Jumatatu ya tarehe ya tarehe 06 Mei 2024 atatoa mikate na siagi kwa Watumishi wote wa ofisi ya Mkoa wa Kusini ili kupunguza adha ya Watumishi hao kutoka ovyo katika zao kutafuta chakula cha Asubuhi

"Watumishi katika Ofisi zetu wamekuwa wakitoa ovyo kwa ajili ya kutafuta chakula hivyo naanza na Ofisi yangu ya Mkoa wa kusini kuanzia Jumatatu ntatoa mikate na Siagi kwa ajili ya chakula cha Asubuhi ili kuongeza ufanisi na kupunguza kutoka hovyo," ameeleza.

Aidha ameeleza kuwa, suala la Watumishi kutoka mara kwa mara katika maeneo yao ya kazi kwa kutafuta chakula linapunguza utendaji kazi wa taasisi mbalimbali.

Hata hivyo RC Ayoub amekemea tabia za uzembe na utoro kwa Watumishi wa taasisi za umma na kiahidi kuwachukulia hatua zinazostahiki.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS