Header Ads Widget

RC AYOUB APIGA MARUFUKU MATUMIZI YA SIMU ZA MKONONI KAZINI


Marufuku matumizi ya simu kazini 


NA MATUKIO DAIMA APP ,ZANZIBAR 

MKUU wa Mkoa wa Kusini Unguja Ayoub Mohammed Mahmoud ametoa agizo la kupiga marufuku matumizi ya Simu na mazungumzo ya binafsi kwa Watumishi wa Umma ndani ya mkoa wa kusini wakati wa kazi.

Agizo hilo amelitoa baada ya ongezeko la malalamiko kutoka kwa Wananchi juu ya Watumishi hao wakitumia muda mwingi wao kazini kuchart na kufanya mawasiliano ya kibinafsi kupitia somu zao za mkononi badala ya kuzingatia majukumu yao ya kazi.

RC Ayoub akizungumza katika Mkutano wa Watumishi wa Umma Mkoa wa Kusini Unguja, amesema kuwa, utendaji kazi wa baadhi ya Watumishi haulidhishi wakati wakiwa kazini muda mwingi hutumia kwa kufanya mawasiliano yao binafsi.

"Ukweli kuwa kuna matumizi mabaya ya ofisi kwa matumishi wa Umma, muda wote wanazungumza na simu,wanachart kwa mambo yao binafsi watakaonekana hatua kali zitachukuliwa dhidi yao," amesema.

"Viongozi Wilaya, Halmashauri na Mabaraza ya Miji na Manispaa hakikisheni munalisimamia hili ili kuboresha ufanisi wa kazi taasisi zenu," ameeleza.

Amesisitiza umuhimu wa Watumishi wa Umma kuzingatia majukumu yao ya kazi wakati wote wa kazi ili kuhakikisha wanatoa huduma bora zenye ufanisi kwa Wananchi.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI