Na Shemsa Mussa,Kagera
Kauli hiyo ikiwa ni moja ya maazimio ya Mkutano wa wadau wa kahawa Mkoa kagera uliofanyika katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo, huku mgeni Rasmi akiwa Bi Hajjat Fatma Mwassa Mkuu wa Mkoa Kagera.
Katika majadiliano ya muda mrefu wadau hao wa kahawa waliweza kutoa maazimio ya kila Halmashauri kuweka mikakati ya namna ya kuzuia biashara ya magendo ya kahawa bila kutumia nguvu ili kulinda mapato ya wakulima na serikali kwa ujumla na pia serikali iwekeze kikamilifu katika Beria, Mialo na Sehemu za mipaka ili kudhibiti utoroshaji wa kahawa.
Pia kusisita kuendelea kutoa elimu kwa wakulima kuhusu madhara ya kuvuna , kuuza na kutorosha kahawa mbichi maarufu kama (Butula) na kusema kuwa msimu wa ununuzi wa kahawa ufunguliwe mapema ili kuepuka upotevu wa kahawa zilizokomaa pia kuongeza ubora na tija ya zao hilo.
Katika Mkutano huo wa kujadili Masuala mbalimbali yanayolihusu zao la kahawa huku Mkuu wa mkoa huo aliweza kuitaja bei mpya ya msimu huu kuwa kila mkulima atauza kahawa kwa bei ya shilingi 3,700 kwa kilo moja ili kuendelea kukuza uchumi zaidi hasa kwa wakulima.
Aidha amesema kuwa katika kuhakikisha wanainua zao hilo wanatarajia kutenga Mashamba ya pamoja hekta 4,000 sawa na hekari 10,000 kwa ajili ya kilimo cha kahawa
Hajjat Fatma ,ameongeza kuwa kwa mwaka 2024/2025 wanatarijia kukusanya Tani 74,000 za kahawa na katika kufanikisha hilo wanatarajia kugawa Miche 5,000 kwa wakulima.
Kwa upande wake Mjumbe wa Halmashauri kuu taifa wa chama cha Mapinduzi CCM Bw Khalim Amri amewataka wadau wa kahawa Kagera kushirikiana kwa pamoja kuyatekeleza yote yaliyojadiliwa ikiwemo wanunuzi kununua kahawa kwa wakati.
0 Comments