Header Ads Widget

MZEE WA MIAKA 60 MATATANI KWA KUBAKA MTOTO WA MIAKA NANE

 



Na Ashton Balaigwa, Morogoro
POLISI Mkoani Morogoro imemtia mbaroni ,Thomas Winga (60), mkulima na mkazi wa Kata ya Kiberege , wilaya ya Kilombero kwa tuhuma za kumbaka  mtoto wa miaka nane.


Kamanda wa Polisi wa mkoa huo , Alex Mkama amesema  tukio hilo  lilitokea Mei 18, 2024 katika eneo la Kiberege , wilayani Kilombero.


Mkama amesema kuwa mtuhumiwa huyo alifanya kitendo hicho baada ya kulaghai mtoto huyo kwa machungwa kisha kumbaka.


Kamanda wa Polisi wa mkoa amesema  kuwa baada ya kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo upelelezi inaendelea kufanyika na mara utakapokamilika atafikishwa Mahakamani kwa hatua zaidi.


Katika hatua nyingine , watu wanne wamekamatwa kwa tuhuma za kujihusisha na matukio ya uporaji simu  kwenye maeneo mbalimbali kwa kutumia pikipiki maarufu Vishandu  na uhalifu mwingine .


Kamanda Mkama amewataja baadhi ya watuhumiwa waliokamatwa ni Samweli Alex (25), Michael Juma (23), Dereva wa Bodaboda mkazi wa Mbuyuni , Iqram  Kuwiga (20) mkazi wa Azimio Manispaa ya Morogoro.


Katika hatua nyingine Polisi  wa kushirikiana na wadau wengine wa matukio ya moto inafanya  uchunguzi wa tukio la kuchoma nyumba moto linalodaiwa kufanywa na Paschal Paul (18), ambalo lilitokea katika kijiji cha Gonja , kata ya Pemba , wilaya ya Mvomero  na kusababisha majereha yake na ndugu zake watatu.


Kamanda wa Polisi wa mkoa  amesema kuwa  tukio hilo lilitokea Mei 19, 2024 majira ya saa mbili usiku katika kijiji hicho  ambapo inadaiwakuwa  mtuhumiwa  amewakusanya ndugu zake watatu kwa lengo la kuwapasha habari .


Mkama amesema , badala yake aliwamiminia kimiminika kilichodhaniwa kuwa ni mafuta yenye asili ya mlipuko na kusababisha kuunguza nyumba yao  ya  nyasi na kusababaisha majereha kubwa kwake na ndugu zake watatu.


Kamanda wa Polisi wa mkoa huyo alisema kuwa  majeruhi wote wamelezwa katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Morogoro.


Aliwataka  maheruhi hao ni Mathias Elias (34) mkulima , Augostino Elias ( 24) mkulima na Anjela Elias (12) mwanafunzi  na wote ni wakazi wa kijiji cha Gonja , kata ya Pemba , wilaya ya Mvomero.


Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa mkoa huyo kuwa , inadhaniwa   mtuhumiwa aliyehusika na kitendo hicho alikuwa na changamoto ya afya ya akili kwa muda mrefu.
Mwisho.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI