Header Ads Widget

MBUNGE PROF. NDAKIDEMA ACHAMBUA ELIMUYA VYUO VIKUU NCHINI…

 


NA WILLIUM PAUL.


MBUNGE wa Jimbo la Moshi vijijini mkoani Kilimanjaro, Prof. Patrick Ndakidemi ametoa ushauri kwa Bodi ya mikopo nchini kuongeza nguvu katika ufwatiliaji wa mikopo ambayo wamekwishaitoa ili kuweza kurejeshwa kwa fedha hizo ziweze kuwasaidia Wanafunzi wengine.

 

Mbunge huyo alitoa kauli hiyo jana wakati akichangia bajeti ya Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia ambapo aliipongeza Wizara hiyo chini ya Waziri Prof. Adolf Mkenda ambapo alisema kuwa mwenendo wa Wiraza hiyo ni mzuri.

 

Alisema kuwa, yapo mageuzi makubwa ambayo yamefanywa na Wizara ya Elimu ambapo husimamia vizuri sekta ya Elimu kuanzia shule ya msingi, sekondari na Vyuo.

 

Alisema kuwa, kwenye kutoa mikopo Bodi hiyo irudi nyuma na kuangalia programa ambapo walikuwa wakitumia kuwapa mikopo kama Madaktari na watu wa sayansi wasije kuacha mtu kwani wao ndio wanaokuja kulisaidia Taifa.

 

“Wizara yetu ya Elimu imepata kiongozi bora na mchapa kazi msikivu , mnyenyekevu mwenye upendo na mshikamano wa hali ya juu na Wabunge wenzake” alisema Prof. Ndakidemi.

 

Alisema kuwa, lengo la mzazi yeyote anayempelekea mtoto wake chuoni ni kuhakikisha kuwa anapata elimu bora, ujuzi, uzoefu na mwishoni anakuwa na mafanikio kwa kuajiriwa au kuwa mjasiriamali hivyo ni vyema taasisi zote ambazo zimepewa dhamana ya kuwapa vijana elimu zikawa zimekamilika kikamilifu.

 

Mbunge huyo alisema kuwa, takwimu walizonazo zinaonyesha kwamba Taasisi nyingi hasa za Serikali na binafsi hapa nchini hazijakamilika ambapo zinaupungufu wa hali ya juu.

 

Alisema kuwa, kutokana na kutokukamilika kwa taasisi hizo kunaupungufu mkubwa wa Waadhiri kumepelekea ufundishaji, utafiti na kutoa huduma kwa jamii kumeathirika kwa kiwango kikubwa.


“Katika vyuo 100 bora Afrika, chuo kikuu cha Nairobi ni cha saba kwa ubora Afrika na ni cha 855 Duniani lakini Makerere ni cha 13 Afrika na ni cha 1613 Dunia, huku chuo Kikuu cha Dar es salaam(UDSM) ni cha 37 Afrika lakini ni cha 2475 Duniani huku chuo kikuu cha SUA ni cha 86 Afrika, huku Chuo cha Afya Muhimbili ni cha 95 Afrika lakini ni cha 4642 Duniani” alisema Prof. Ndakidemi.

 

Alisema kuwa, katika vyuo kumi bora Afrika vyuo saba vinatoka Afrika kusini na kimoja kimetoka Afrika mashariki, huku katika vyuo 100 bora Afrika vyuo kumi vimetoka Afrika mashariki.

 

Aliishauri Serikali kuwekeza kikamilifu kwenye uendeshaji wa vyuo vikuu nchini vipewe fedha ya kutosha ili wahitimu wa vyuo hivo wawe bora na kutoa taswira ya kutoa wasomi wa uhakika ili wawe na uhakika wa ushindani.

 

Ameitaka Serikali kuwa na programu ya kuwasomesha vijana na kuwaendeleza kuwa na PHD za uhakika hasa kuwapeleka kusoma nje ili kupata ujuzi, pili serikali isifungue kampasi mpya hadi isomeshe vijana wa kutosha na kuwapeleka katika kampasi hizo.

 

Mwisho…

 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS