Na Ashton Balaigwa,MOROGORO
JESHI la Polisi mkoani Morogoro limefanikiwa kuwatia mbaroni madereva 10 kwa tuhuma za makosa ya usalama barabarani akiwemo dereva wa Lori ,Samsoni Uwiringiyimana (35), raia wa Rwanda anayetuhumiwa kwenye tukio la ajali iliyosababisha vifo vya watu saba na kujeruhi wengine sita iliyotokea siku ya Jumanne wiki hii.
Kamanda wa Polisi wa mkoa huo , Alex Mkama amesema kuwa madereva hao wamekakatwa katika operesheni za usalama barabarani zinaendelea kufanyika mkoani Morogoro.
Mkama amesema Samsoni alikuwa akiendesha gari la mizigo aina ya MAN lenye namba za usajili RS 980 X3 ambalo liligongana uso kwa uso na gari ndogo ya abiria aina ya Noah yenye namba za usajili T 101 DKB.
Amesema tukio hilo lilitokea Mei 14,mwaka huu (2024) ,majira ya saa mbili na nusu asubuhi eneo la Dakawa , wilaya ya Mvomero wakati gari hilo dogo la abiria ikiwa inatokea Mji wa Dumila ,wilayani Kilosa kuelekea Morogoro mjini, na Lori hilo la masafa marefu ililikuwa linatokea Morogoro mjini kwenda Dodoma.
Kamanda huyo wa Polisi wa mkoa alieleza ya kwamba baada ya kutokea kwa ajali hiyo Dereva wa Lori alilimbia kusikojulikana na kulitelekeza gari lake na kwamba Polisi waliazisha msako wa kumtafuta ili atakapopatikana aweze kuchukuliwa hatua za kisheria na kufikishwa mahakamani.
MWISHO.
0 Comments