NA MATUKIO DAIMA APP
MAANDAMANO ya chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) yaliyoongozwa na makamu mwenyekiti wa chama hicho Tanzania bara Tundu Lissu jana yameshindwa kufanyika kama ilivyopangwa kuanza katika kanda mbili tofauti kwa kile kilichoelezwa kuwa kukosa kibali cha kufanyika kwa njia mbili kama ilivyopangwa mwanzo .
Awali maandamano hayo yalitangazwa kufanyika kuanzia kanda ya Kihesa na kanda ya Mlandege ambako Tundu Lissu ndie aliyekuwa kiongozi wa maandamano hayo bila kutaja sababu ya kutofanyika kwa maandamano kanda ya Kihesa mwenyekiti wa chadema jimbo la Iringa mjini Frank Nyalusi alisema wamezuiwa kutumia njia ya Kihesa na kuruhusiwa kufanya maandamano njia moja pekee ya Mlandege hadi viwanja vya Mwembetogwa .
Nyalusi alisema kuwa kuwa maandamano hayo ni mwanzo wa maandamano na mkutano mkubwa wa Chadema mkoa wa Iringa ambao utakuja fanyika katika viwanja hivyo vya mwembetogwa na kuwa maandalizi ya maandamano hayo ni ya siku moja pekee na ndio sababu ya watu kutokuwa wengi zaidi japo kubwa ni kufikisha ujumbe wa serikali juu ya hitaji la msingi la kudai katiba mpya .
Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Mwembetogwa Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Nyasa mchungaji Peter Msigwa alisema kuwa sababu kubwa ya kuandamana ni kudai katiba mpya pamoja na kuiambia serikali juu ya ugumu wa maisha kwa watanzania .
Kuwa wapo baadhi ya watu wanabeza Maandamano ya Chadema kuona kama Maandamano hayo hayawahusu ila nao ni miongoni mwa watu wanaokosa Haki kutokana na katiba mbovu na pia wanalia ugumu wa maisha kwa kuendelea kushuhudia gharama ya bidhaa zikiendelea kupaa Siku hadi siku.
"Naomba kuwaambia watanzania Maandamano haya si ya Chadema Pekee ni Maandamano ya watanzania wote maana katiba mpya si ya Chadema ni ya Taifa Zima"
Kwa upande wake John Heche alisema kuwa Chadema inaomba watanzania wote kuunga mkono Maandamano hayo kwani hivi sasa Chadema inaugulia maumivu kwa kukimbiwa na wenyeviti wa serikali za mitaa pamoja na wabunge na madiwani ambao walinunuliwa na serikali ya CCM .
Alisema kuwa serikali ya awamu ya sita chini ya hayati John Magufuli iliacha maumivu makubwa ndani ya Chadema kwa kuwanunua wenyeviti na madiwani wake.
Kwa upande wake makamu mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Tundu Lissu anashangaa mabango makubwa yenye picha ya wanawake wa Baraza la wanawake wa Chadema ( BAWACHA ) ambayo yapo nchi Nzima kwenye miji kuwa kuonesha Wao na mama hawana matatizo si kweli .
Lissu akihutubia wananchi wa mji wa Iringa Jana alisema kuwa mabango hayo yanatumika kuwachafua kwa wananchi kuonesha kuwa Chadema na mama hawana tatizo ila ukweli tatizo lipo kwani ndio maana wanaandamana .
"Mabango haya yanatumika kutuchafua kwa wananchi kuwa sisi na serikali hatua tatizo ama kuonesha tumehongwa ila ukweli mabango haya hata sijui kwanini tulimualika ila haina shida ukweli CHADEMA tunaandamana kwa kuwa tuna ona shida ipo kubwa tunaandamana kudai katiba mpya"
Katika hatua nyingine Lissu amesikitishwa na ukimya wa serikali baada ya benki ya Dunia kusitisha kutoa pesa kiasi Cha Tsh bilioni 48 kwa ajili ya Hifadhi ya Taifa ya Ruaha kutokana na Hifadhi hiyo kunyanyasa wananchi .
Lissu alisema kwa sasa sehemu nyingi wananchi wamekuwa wakilalamika kunyanyasika kwenye ardhi yao huku serikali ikiwa kimya huku wananchi wakilia kukosa ardhi ila nchi Nzima mabango yakiwekwa kuonesha nani kama mama.
0 Comments