Header Ads Widget

EWURA KANDA YA MAGHARIBI KUENDELEA KUTEKELEZA MAJUKUMU YAKE KWA WELEDI

Meneja wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Kanda ya Magharibi  Walter Christopher akizungumza wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga yaliyoandaliwa na EWURA kwa kushirikiana na Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (SPC).

Na Mapuli Kitina Misalaba

Meneja wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Kanda ya Magharibi Walter Christopher amesema mamla hiyo itaendelea kutekeleza majukumu yake kwa weledi, uwazi na ushirikishaji ili kuimarisha huduma za nishati na maji kwa manufaa ya taifa.

Akizungumza leo Mei 2,2024 kwenye semina na waandishi wa habari wa Mkoa wa Shinyanga ambayo imeratibiwa na EWURA kanda ya Magharibi kwa lengo la kuongeza  uelewa kuhusu majukumu ya mamlaka hiyo.

Meneja huyo ameeleza kuwa EWURA itaendelea kusimamia watoa huduma za Nishati na Maji ili kuhakikisha huduma zinakuwa bora kwa manufa ya taifa.

“Sisi EWURA tutaendelea kutoa ushauri kwa serikali katika kuandaa sera, sharia na kanuni zitakazowezesha kukua kwa sekta za Nishati na Maji na kuendelea kusimamia watoa huduma ili kuhakikisha huduma zinakuwa bora kwa manufaa ya taifa”.

“Lakini pia tutaendelea kuzingatia misingi mikuu sita ya utawala bora katika maamuzi ya udhibiti ambayo ni weledi, uwajibikaji, utabirikaji, ushirikishaji, uwazi na kufuata sharia”.amesema Christopher

Wakati huo huo amesema kuwa waandishi wa habari ni kundi muhimu na kwamba wakielimishwa vizuri na kuwa na uelewa wa kutosha wataandika habari zao kwa usahihi na kuhabarisha umma.

Kwa upande wake afisa kutoka idara ya Mafuta EWURA Mhandisi Ibrahim Kajugusi amesema kuwa Mamlaka ya udhibiti wa huduma za Nishati na Maji EWURA inaendela kuwahamasisha wafanya biashara kufungua vituo vya Mafuta vijijini ili kukabiliana na uuzaji holela wa Mafuta.

Pia amesema ni kosa kisheria kwa mtu yeyote kufanya biashara ya Mafuta bila kuwa na Leseni kutoka kwenye mamlaka husika na kwamba hatua za kisheria zinaweza kuchukuliwa kwa mtu huyo.

Kwa upande wake afisa mahusiano mwandamizi kutoka EWURA Tobietha Makafu ameeleza majukumu na kazi za EWURA ambapo amesema mamlaka hiyo imefanikiwa kudhibiti uchakachuaji wa Mafuta.

Naye afisa mwandamizi huduma kwa wateja EWURA kanda ya Magharibi Bi. Getrude Mbilingi ameeleza utaratibu wa kuwasilisha malalamiko kwenye mamlaka hiyo huku akiwahimiza watumiaji wa Nishati na Maji wenye changamoto kutoa taarifa ili ziweze kushughulikiwa haraka.

Mjumbe wa kamati ya watumiaji wa huduma za Nishati na Maji kutoka EWURA CCC Bwana Joseph Ndatala amesema baraza hilo litaendelea kutetea na kulinda maslahi ya watumiaji wa huduma za Nishati na Maji zinazodhibitiwa na EWURA.

Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoa wa Shinyanga, Bw. Patrick Mabula, ameishukuru na kuipongeza EWURA kwa semina hiyo na kuahidi kuwa elimu hiyo wataitumia kuelimisha wananchi kupitia vyombo vyao vya habari.

Mafunzo hayo yamehudhuriwa na waandishi wa habari kutoka katika vyombo mbalimbali vikiwemo Magazeti, Redio, Televisheni na vyombo vya habari vya mtandaoni (Blogs & Online Tv).

EWURA Kanda ya Magharibi  inahudumia Mikoa ya Tabora, Shinyanga, Katavi na Kigoma leo imetoa  mafunzo kwa Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga kwa lengo la kuwajengea uelewa juu ya Majukumu ya EWURA na Kazi za Ofisi ya Kanda hiyo.

Meneja wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Kanda ya Magharibi  Walter Christopher akizungumza wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga yaliyoandaliwa na EWURA kwa kushirikiana na Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (SPC).

Afisa kutoka idara ya Mafuta EWURA Mhandisi Ibrahim Kajugusi akizungumza wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga yaliyoandaliwa na EWURA kwa kushirikiana na Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (SPC).













Mwandishi wa habari Kareny Masasy akizungumza kwenye semina hiyo.

 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS