Header Ads Widget

WIZARA YA MAMBO YA NDANI YAJIVUNIA UBORESHAJI MKUBWA WA OFIS, MAKAZI YA ASKARI

 

Na Hamida Ramadhan Matukio Daima App Dodoma

IMEELEZWA Kuwa Umefanyika uboreshaji mkubwa wa Ofisi na Makazi ya askari wa Vyombo vya Usalama vya Muungano ambapo kwa sasa Wizara imebadilisha mfumo wa ujenzi wa nyumba za askari wa vyeo mbalimbali kutoka kuwa nyumba za mabati na kuwa nyumba za kisasa. 

Hayo yamesemwa leo jijini hapa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi Hamadi Masauni wakati alipokuwa kwenye mikutano wake na waandishi wa habari,

Amesema hadi sasa Jeshi la Polisi limejenga nyumba ni 10,450 kwa ajili ya makazi ya askari wake. Pia zimejengwa Zahanati za Jeshi la Polisi 35 katika Mikoa mbalimbali nchini ambazo huduma za matibabu kwa askari wa Jeshi la Polisi, familia zao na raia wa kawaida. 

Amesema Kwa upande wa Idara ya Uhamiaji Serikali imeiwezesha kujenga nyumba 454 kwa ajili ya makazi ya Maafisa, Askari na watumishi wake katika Mikoa mbalimbali nchini, ukilinganisha na majengo machache ya Makazi yaliyokuwepo kabla ya Muungano mwaka 1964. 

"Ujenzi wa makazi ya Askari umesaidia kuwaweka sehemu moja na kuwa rahisi kupatikana kwa haraka pale wanapohitajika kwa dharura. Pia, umesaidia kupunguza gharama kwa askari ya kupanga uraiani na kuongeza usalama zaidi kwa askari, " Amesema Mhandisi ,Waziri Masauni

Na kuongeza "Uwepo wa makazi hayo umepunguza malalamiko kutoka kwa wananchi kuwa askari wanapoishi katika nyumba za uraiani huwafanya kushindwa kutimiza majukumu yao ipasavyo kwa kuhofia usalama wao na familia zao, " Amesema .

Aidha Katika kipindi cha miaka 60 ya Muungano wa Jamhuri ya Tanzania, Jeshi la Polisi limefanikiwa kujenga Vituo vya Polisi 485 vya daraja ‘A’, ‘B’ na ‘C’ pamoja na ofisi 20 za Makamanda wa Polisi katika Mikoa mbalimbali nchini.

 Amesema, Idara ya Uhamiaji imefanikiwa kujenga majengo yake ya Ofisi 65 na kuwa na Ofisi katika Mikoa 31, Wilaya 134 na Vituo 64 vya kuingia na kutoka nchini kwa upande wa Bara na Visiwani, ukilinganisha na vichache vilivyokuwepo kabla ya Muungano.

Ujenzi wa Vituo vya Polisi umesaidia kusogeza huduma za polisi kwa wananchi na kuwafanya wananchi kupata fursa ya kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu kwani zamani huduma hizo walikuwa wanazipata kwa kutembea umbali mrefu na kuwafanya kubaki na taarifa za matukio waliyosikia au kuona kutokana na kushindwa kuyafikisha kwenye Kituo cha Polisi kwa kuhofia kutembea umbali mrefu kwenda kutoa taarifa.  


POLISI JAMII :

Katika kuondokana na mfumo tuliorithi wa kikoloni, Jeshi la Polisi katika Maboresho yake limeanzisha programu ya Polisi Jamii. Programu hiyo ndani yake kuna miradi takribani 25 inayotekelezwa Tanzania nzima ikiwepo Ushirikishwaji wa Jamii; Ulinzi Shirikishi; Polisi Kata; Usalama wetu Kwanza; na Dawati la Jinsia na Watoto. 


Miradi hiyo imewafanya wananchi kuwa na imani na Jeshi la Polisi na kuwa karibu na hivyo kuwezesha utendaji wake ikiwemo kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu na kuanzisha vikundi vya ulinzi shirikishi katika mitaa. 


Amesema Polisi jamii imelisaidia Jeshi la Polisi kuwa na uwezo zaidi wa kubaini na kuzuia uhalifu na kuweka mazingira rafiki baina ya polisi na wananchi katika kupata taarifa za matukio mbalimbali kwenye jamii na kuongeza ufanisi katika majukumu yao.


Jeshi la Polisi limefanikiwa kupeleka Polisi Kata 2,608 wenye cheo cha Mkaguzi na Mkaguzi Msaidizi kwenye Kata zote za Tanzania Bara  na askari wa vyeo mbalimbali 1,353 na  kwa upande wa Zanzibar na wakaguzi 169 na askari wa vyeo mbalimbali 134 wamepangwa kwenye shehia.


Polisi Kata wamesaidia kuwajengea uelewa wananchi kuhusu kubaini, kuzuia na kutanzua uhalifu; na

Kusaidia kutatua kero za kiusalama kulingana na mazingira ya eneo husika (local problem for the local solution).


Mwisho

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI