NA AMINA SAIDI,TANGA
HALMASHAURI ya jiji la Tanga imewawezesha makundi mawili ya wazazi wenye watoto wanaoishi na ulemavu kwa kuwasaidia kiasi cha shilingi milioni kumi na nane (18,000,000)kutoka katika mapato ya ndani.
Hayo aliyasema Afisa ustawi wa jamii jiji la Tanga Hossein Mshana wakati kiongozi wa mbio za mwenge wa Uhuru Kitaifa alipotembelea na kujionea shughuli za uwezeshaji wa watu wenye ulemavu katika kituo jumuishi cha watoto na vijana wenye ulemavu (YDCP).
Mshana alisema kuwa Halmashauri imewawezesha vijana sita wa kike mmoja na wakiume watano wenye ulemavu kwa kuwapatia mkopo wenye thamani ya shilingi milioni sita na laki tano ambapo tayari wameshaanza kurejesha asilimia sabini na saba.
Sambamba na hayo Halmashauri ya jiji la Tanga kwa kushirikiana na Asasi za kijamii na vikundi mbali mbali katika katika kutoa elimu dhidi ya mapambano ya ukatili wa kijinsia na ukatili kwa watoto katika kata zote 27 na mitaa 181,ambapo elimu hiyo imekuwa ikitolewa na wataalamu mbalimbali wakiwemo maafisa wa jamii.
Hata hivyo hatua zilizochukuliwa dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia ni pamoja na kuwafikisha mahakamani na kuhukumiwa.
Katika kipindi cha mwaka 2023 mpaka sasa jumla ya kesi 20 zilifikishwa mahakamani ambapo miongoni mwa kwesi hizo ,kesi 12 watuhumiwa wamwhukumiwa adhabu ya kifungo na bado kesi 8 zinaendelea.
Halmashauri ya jiji la Tanga lina jumla ya watu wenye ulemavu 1,236 kwa kwa kushirikiana na wadau imeibua watu wenye usonji,uziwi,kichwa kikubwana utindio wa ubongo.
Katika utoaji wa huduma hizo Halmashauri ya jiji la Tanga imekuwa ikitoa elimu katika shule za msingi Majani mapana( ulemavu wa akili)Shule ya msingi Bweni Pongwe (ulemavu wa macho na albino)shule ya msingi Chuda( ulemavu wa kusikia)shule ya msingi Usagara na Mwakidila (ulemavu wa akili)na huduma za utengamao katika kituo jumuishi cha watoto na vijana wenye ulemavu(YDCP).
0 Comments