Na, Matukio daima App Lindi
Watu 13 wamefariki dunia na wengine wamejeruhiwa kufuatia ajali y abasi dogo la abiria aina ya coster iliyokuwa ikitokea Somanga kuelekea Kilwa Kivinje kugongana uso kwa uso na Lori la mafuta.
Kamanda wa Jeshi la polisi mkoa wa Lindi, John Imori amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo majira ya saa mbili asubuhi, katika barabara kuu ya Somanga – Nangurukuru huku akisema zaratibu zingine za kubaini chanzo cha ajli hiyo zinaendelea.
Majeruhi wote wamepelekwa katika Hospital ya Tingi kwa ajili ya Matibabu zaidi huku miili yote 13 imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti, katika hospital ya hiyo.
0 Comments