Header Ads Widget

WAKULIMA WA KARANGA MKINGA NA MAGU WAFURAHIA UTAFITI SHIRIKISHI

 Na Mwandishi wetu, Matukiodaima app

 


Wakulima wa zao la karanga kutoka Wilaya za Mkinga na Magu wamefurahia utafiti shirikishi kwa zao la karanga ambao umeleta manufaa kwao hali ambayo imewahamsisha zaidi kulima zao hilo.

Akizungumza mara baada ya kupata mafunzo kutoka Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania-TARI kituo cha Naliendele  Dau James mkulima wa zao la Karanga Wilayani Magu Mkoani Mwanza amesema kuwa zao la karanga limekuwa zao mkombozi kwao.

Amesema kuwa zao hilo ni zao ambalo mkulima akifuata ushauri wa watafiti na akalima kitaalamu tunaweza kubadilisha maisha yetu shambani.

“Hasa hii mbegu aina ya Mangaka imetupiendeza tumesabaza hadi kwa wakulima ambao sio wanakikundi ili waweze kulia mbegu hii kwakweli inazaa watoto zaiid ya wanne mavuno yake yanashawishi wakulima kulima  zao litakuwa na nafasi kubwa ya kuweza kulimwa kwa wingi katika kijiji chetu”


Uba Mwalimu amesema kuwa watafiti wametoa maelekezo naamini ili zao hili liwe na tija tunapaswa kuzingatia ushauri wao.

“Waswahili walisema jembe halimtupi mkulima hata kilimo hakitupi yaani ukilima vizuri na ukizingatia maelekezo ya watalaamu utavuna mazao mengi na utauza na kupata pesa”

Mtafiti wa Kilimo TARI Naliendele Gerald Alex amesema kuwa elimu hiyo itasaidia wakulima kuongeza zalishaji na kuanza kulima zao hilo kama zao la kibishara.

“Tumesambaza mbegu bora kwenye mashamba darasa ili wajifunze aina ya mbegu bora  tulizonazo na namna zinavyoweza kufanya vizuri katika mashamba yao” alisema Gerald

“Ipo mikakati ya tuliyoweka Tari kituo cha Naliendele ili kuhakikisha kuwa wa tafiti na mbegu zinazo zalishwa na kituo chetu zinawafikia wakulima ili mipango ya serikali ya kukuza sekta ya kilimo inafanikiwa ambapo sasa katika maeneo yenye fursa ya kulizalisha zao hilo yanafikiwa na kufanytafiti shirikishi” amesema Gerald

Nae Julius Butindi Mtafiti wa Kilimo TARI Nalindele amesema kuwa kupitia mashamba darasa wakulima wengi wamefurahia na kulizishwa na aina mbalimbali za mbegu ikiwemo Mangaka.

“Unajua aina hii ya Mangaka inazaa kwa wingi inaweza kufikia tani moja na nusu kwa hekta inazaa kuanzia watoto watatu hadi wanne ni mbegu ambayo wakulima wakiizingatia wanaweza kupata tija zaidi” alisema Butindi  

Afisa Kilimo Halmashauri ya Wilaya ya Magu Alfonce Awaki amesema kuwa uwepo wa mbegu za karanga zinazofanya vizuri kwetu ni faraja kubwa kwakuwa sasa tumepata zao mbadala.

“Sisi kama Wilaya tunapambana kupata zao mbadala tukipata mbegu bora tutakuwa tumepata zao mbadala ili kuongeza kipato cha mkulima wetu na pita tunaamini kuwa wakulma wataongezeka na kuleta tija zaidi” amesema Awaki

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga Rashidi Gembe amesema kuwa hili kwetu ni zao jipya ni fursa mpya.

“Yaani tutahamsisha wakulima wachangamkie fursa hii ya kilimo cha karanga iwe ni zao jipya la kibishara ili kuweza kuongeza kipato chao na Halmashauri kwa ujumla” amesema Gembe


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI