Marekani imesitisha baadhi ya shehena za silaha kwenda Kyiv, Ikulu ya Marekani imesema, huku vita vya Urusi dhidi ya Ukraine vikizidi kupamba moto.
Uamuzi huo ulichukuliwa "kuweka masilahi ya Marekani mbele" kufuatia tathmini ya Idara ya Ulinzi kuhusu "msaada wa kijeshi na usaidizi wa Marekani kwa nchi zingine", msemaji wa White House Anna Kelly alisema Jumanne.
Marekani imetuma makumi ya mabilioni ya dola ya misaada ya kijeshi kwa Ukraine tangu Urusi ilipoanzisha uvamizi wake mwezi Februari 2022, na kusababisha baadhi katika utawala wa Trump kueleza wasiwasi wao kuwa akiba ya silaha ya Marekani ni ndogo sana.
Serikali ya Ukraine haijatoa maoni yoyote kuhusu tangazo hilo. Maafisa wa Marekani hawakusema mara moja ni usafirishaji gani uliokuwa ukisitishwa.
0 Comments