NA HAMIDA RAMADHAN, MATUKIO DAIMA APP DODOMA
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dkt.selemani Jafo amesema kuwa wakati taifa linaelekea kuadhimisha miaka 60 ya Muungano ambapo viongozi wa dini kutoka madhehebu mbalimbali zaidi ya 100 wamefika Dodoma kwa kitumia Treni ya kisasa ya umeme wa majaribio kutoka Dar el Salaam
Akizungumza mara baada ya kuwapokea viongozi hao jijini hapa leo,Aprili 21,2024,
Waziri huyo akiwa na viongozi wengine mbalimbali akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Rosemary Senyamule pamoja na wananchi amesema kuwa viongozi hao wanatarajiwa kushiriki ibada maalum ya kuliombea Taifa katika uwanja wa Jamhuri leo Aprili 22,2024 wakiongozwa na Makamu wa Rais Dkt.Philip Mpango.
Amesema suala la viongozi wa dini kusafiri kwakutumia treni ya kisasa ya umeme ni mafanikio makubwa na serikali imeona ni vyema viongozi wa dini kuwa wa kwanza kusafiri na usafiri huo wakiwa wanaenda kuliombea Taifa.
"Ndugu zangu najua mmetoka mbali tunawakaribisha sana Dodoma lakini naomba niwambie viongozi wa dini serikali inayoongozwa na Dkt.Samia inawapenda sana na kesho tutakuwa na maombi ya kuliombea Taifa letu kwa tunu ya Muungano tulionao,"amesema Dkt.Jafo.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu Shirika la Reli Tanzania(TRC)Masanja Kadogosa amesema kuwa wanaposafiri na treni hiyo wanatesti madaraja kuhakikisha ubora wake upo vizuri pamoja na makaravati.
Aidha amesema kuwa Treni hiyo ya umeme iliyobeba watu mbalimbali pamoja na viongozi wa dini 160 imetumia umeme wa shilingi milioni 1.2 kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma kwa saa 3 na dakika 21.
MWISHO
0 Comments