Mawasiliano kati ya Ifakara na Mlimba yamekatika na kusababisha mamia ya wasafiri kushindwa kuendelea na safari baada ya Kalavati kusombwa na maji yaliyotokana na mvua zinazoendelea kunyesha hapa nchini.
Akizungumzia tukio hilo leo April 2, 2024 meneja wa wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) mkoa wa Morogoro, Alinanuswe Kyamba amesema jitihada za kurejesha mawasiliano zinaendelea.
“Ni kweli Aprili mosi tulipata changamoto ya barabara inayounganisha Ifakara na Mlimba kukatika baada ya Kalavati inayounganisha maeneo hayo kusombwa na maji, ni kweli kwa sasa eneo lile huwezi kupita kutoka upande mmoja Kwenda mwingine, hiyo ni kutokana na maji kuwa mengi lakini jitihada za kurejesha hali ya kawaida zinaendelea kutoka kwa wataalamu wetu” amesema Kyamba.
“Tayari timu
ya mafundi kutoka mkoani hapa
na wale wa mlimba penyewe, wameshafika eneo
lililokatika na tumeshapeleka mitambo kwa ajili ya kusaidia kuondoa vifusi na
mawe ambayo yameziba eneo lile baada ya Daraja kusombwa na maji” amesema Kyamba.
Hata hivyo, amewataka wananchi wa Ifakara na Mlimba kuwa wavumilivu kwa kipindi hiki ambacho Tanroads na wataalamu wake wanaendelea kushugulikia tatizo hilo.
“Niwaombe wananchi wa maeneo hayo wawe watulivu maana tunafanya kazi usiku na mchana kuona hali inarudi kama zamani”.
0 Comments