Header Ads Widget

TOPE LA KWAMISHA USAFIRI WA TRENI KATIKA RELI YA TAZARA KILOMBERO

 

 


Usafiri wa treni katika reli ya Tazara umesimama kwa muda usiojulikaan baada ya eneo la Kijiji cha Lumumwe, wilayani Kilombero, Mkoani Morogoro, kunapopita treni hiyo kujaa tope kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha.

 

Akitoa taarifa hiyo leo jumanne April 2, 20224, mkuu wa wilaya ya Kilombero, Danstan Kyobya amesema changamoto hiyo imetokea jana na tayari kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya pamoja na kamati ya uokozi zimefika eneo hilo ili kuhakikisha hali ya usafiri inarejea kama kawaida.

 

“Ni kweli Usafiri umesimama baada ya reli ya Tazara Kijiji cha Lumumwe kujaa tope, hata hivyo tayari wataalamu wameshafika katika eneo hilo na wanaendelea na kazi”.

 

Hata hivyo, Kyobya amehaidi kutoa taarifa kamili ikiwemo ya idadi ya abiria walioshindwa kuendelea na safari kutokana na changamoto hiyo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI