Header Ads Widget

UNICEF WAKABIDHI MSAADA WA VIFAA VYA SHULE KWA WANAFUNZI NA WALIMU KWA SHULE ZILIZOATHIRIKA NA MAFURIKO KIBITI NA RUFIJI

 

Shirika la Kimataifa la kuhudumia watoto duniani UNICEF limetoa msaada wa vifaa vya Shule za msingi na Sekondari kwa Shule zilizoathirika na mafuriko katika Wilaya za Rufiji na Kibiti mkoani Pwani ambapo Wanafunzi 1040 na Walimu vyenye thamani ya Dola 9586.20 Mwandishi  Scolastica Msewa anaripoti kutoka Rufiji


Alikabidhi Msaada huo Mkuu wa kitengo Cha Elimu maalumu wa wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Magreth Matonya kwa Mkuu wa mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge ambaye aliwakirishwa na Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Meja Edward Gowele alisema vifaa vilivyotolewa ni kwaajili ya Shule 14 zilizoathirika na mafuriko kwa Wilaya za Rufiji na Kibiti.

Alisema Msaada huo utapelekwa kwenye shule hizo ambazo maji ya Mto Rufiji yamejaa ambapo Wanafunzi hawawezi kuendelea na masomo na vifaa vyao vimeharibika kwa namna Moja au nyingine na mafuriko hayo yanayoendelea wilayani humo.


Dkt. Matonya alitaja aina ya vifaa hivyo vya Shule vilivyoletwa kuwa ni pamoja na mahema ya kutengeneza madarasa 4, vifaa vya kusomea Wanafunzi, vifaa vya kufundishia kwa Walimu,  vifaa vya michezo na vifaa vya Wanafunzi wenye mahitaji maalumu.


Alisema katika mahema hayo matatu yatapelekwa kwaajili Shule 7 zilizofungwa wilaya ya Rufiji na hema moja litakabidhiwa kwaajili ya Shule zilizofungwa wilayani Kibiti.


Akipokea Msaada huo Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Meja Edward Gowele alishukuru UNICEF kwa msaada huo na kusema Wilaya za Rufiji na Kibiti Ina shule 23 zilizoathirika na mafuriko hayo huku shule 14 zimefungwa kwa athari za mafuriko hayo kwa Wilaya zote mbili.


Akipokea Msaada huo kwaajili ya Wilaya ya Kibiti Mkuu wa Wilaya ya Kibiti Kanali Joseph kolombo alishukuru serikali na wizara ya Elimu, UNICEF kwa msaada huo na kwamba vifaa hivyo vitasaidia Wanafunzi wa Shule wa Shule tatu wilizofungwa kabisa kwasababu ya mafuriko hayo.


Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji Simon Belege alisema misaada hiyo itasaidia Wanafunzi wenye mitihani ya kittaifa kuendelea na masomo ili wasipitwe na kuchelewa muda wa mitihani ya kittaifa.


Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti Hemed Magaro alisema haraka wanajenga mahema hayo ili Wanafunzi waendelee na masomo yao kwa kutumia vifaa hivyo.


Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Rufiji Kaswakala Mbonde alionya wanasema mafuriko hayo ni kutokana na kujengwa kwa Bwawa la kuzalisha Umeme la Mwalimu Julias Kambarage Nyerere kwani matukio ya mafuriko katika Wilaya hizo ni zaidi ya miaka hamsini Sasa.


 









Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS