Header Ads Widget

TAKUKURU KAGERA YABAINI MAPUNGUFU KATIKA MIRADI 21 SAWA NA 98.87 YA FEDHA ZILIZOTOLEWA

Na Shemsa Mussa,Kagera 

MKUU wa taasisi  ya kuzuia na kupambana na rushwa Mkoani Kagera Pilly Mwakasege amesema kwa kipindi cha Januari hadi Machi mwaka huu walibaini miradi 21 yenye thamani zaidi ya shilingi bilioni 8.9 kuwa na mapungufu yaliyohitaji marekebisho sawa na asilimia 98.87 ya fedha za miradi hiyo.


Mwakasege ameyasema hayo wakati akiongea na vyombo vya habari ofisini kwake na kusema kuwa kumekuwa na  ongezeko la asilimia 30.37 ya fedha za miradi iliyobainika kwa kuwa na mapungufu katika utekelezaji ukilinganisha na kipindi cha Oktoba hadi Desemba 2023 ambapo mapungufu hayo yalikuwa asilimia 68.50.


Mwakasege amesema katika kipengele cha uchunguzi na mashtaka walipokea malalamiko 110 kati ya hayo 96 hayahusu rushwa hivyo walalamikaji walielimishwa na kupewa ushauri ambapo malalamiko 14 yalihusu rushwa na  kufunguliwa majalada  huku  kumi uchunguzi wake umekamilika,hatua mbalimbali za kisheria zinatarajiwa kuchukuliwa dhidi ya watuhumiwa na majalada manne uchunguzi wake bado unaendelea.


Alizitaja idara zinazolalamikiwa kuwa ni Halmashauri malalamiko (49),Idara ya fedha (10),idara ya elimu (6),kilimo na mifugo (2)watu binafsi (61)Tarura (3),Ushirika (5),Polisi (12),,TFS( 2),Ruwasa (1),TRA (2),UHamiaji (3) Sekta Binafs  (7),Buwasa ( 1).Nps (1),Mahakama (1) na Tanesco (2).

 

"Mfano wa baadhi ya Miradi tuliyofuatilia ni ujenzi wa miundombinu ya Maji, Ujenzi wa Zahanati, Barabara, Shule mpya Ujenzi wa Vyumba vya Madarasa, Matundu ya Vyoo, Bwalo na Mabweni katika Shule za Msingi na Sekondari" amesema Mwakasege.


Aidha wamepokea malalamiko mapya (8) ambayo yamefunguliwa mahakamani na kufanya jumla ya malalamiko kufikia 27 yanayoendelea kusikilizwa  katika mahakama mbalimbali ndani ya Mkoa  Kagera na katika kipindi cha miezi mitatu mashauri (9) yamefanyiwa maamuzi ambapo Jamhuri imeshinda mashauri yote.


Amesema hayo yote yamefanikiwa kutokana na kampeni ya TAKUKURU rafiki ambapo pia  malalamiko yasiyohusu rushwa yameongezeka kutokana na kuongezeka kwa madai kati ya mtu na mtu ambapo wananchi wanaodaiana wao kwa wao wameshauriwa wafuate sheria ya madai kwa mujibu wa mikataba yao ya kukopeshana.


Pia Mkuu huyo amewataka  wasimamizi wa Miradi ya Maendeleo kuwa waadilifu kuhakikisha Fedha zote za Miradi zinatumika vizuri na kuongeza juhudi katika usimamizi wa Miradi husika na kufanya marekebisho ya mapungunfu katika miradi iliyobainika kuwa na mapungufu kwa wakati kama wanavyoshauriwa.


Hata hivyo, amevitaja vipaumbele kwa kipindi cha Aprili hadi Juni kwamba ni kuendelea kufuatilia utekelezaji wa miradi ya maendeleo ili kuziba ufujaji wa fedha za Umma na kuendelea kutatua kero za wananchi kwenye jamii kupitia program ya Takukuru rafiki.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS