Header Ads Widget

SECRETARIET YAKUNA KICHWA MMOMONYOKO WA MAADILI KWA VIONGOZI, WATUMISHI WA UMMA

Na Fadhili Abdallah,Kigoma


ONESMO MSALANGI AFISA MAADILI SECRETARIET YA MAADILI YA UMMA KANDA YA MAGHARIBI

 
SEKRETARIETI ya maadili ya umma imesema kuwa mmomonyoko mkubwa wa maadili kwa watumishi wa umma ni changamoto kubwa katika utoaji huduma bora hivyo imeanza kukabiliana na changamoto hiyo kwa kuunda vilabu vya maadili shuleni ili suala hilo lianze kudhibitiwa kuanzia shule za msingi na sekondari.
 
Afisa maadili kutoka sekretariet ya maadili kanda ya Magharibi, Onesmo Msalangi alisema hayo katika mafunzo ya siku moja kwa walimu walezi wa klabu za maadili katika shule 10 za msingi na sekondari manispaa ya Kigoma Ujiji ambapo sekretariet hiyo inaanzisha klabu za maadili kwenye shule hizo.
 
Msalangi alisema kuwa kwa sasa kuna changamoto kubwa ya maadili kwa viongozi kwenye utumishi wa umma jambo linalofanya kuwepo kwa uvunjifu wa sheria, kanuni,taratibu na miiko ya kazi kwa viongozi ambao wengine wamekabidhiwa na kuaminiwa kusimamia masuala nyeti ya serikali.

HALIMA RAMADHANI AFISA MAADILI SECRETARIET YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA KANDA YA MAGHARIBI


 
Akizungumzia kuanzishwa kwa vilabu vya maadili mashuleni Afisa Maadili kutoka Sekretariet ya maadili ya viongozi kanda ya Magharibu, Halima Ramadhani alisema kuwa kuna ombwe kubwa kwa viongozi na watumishi  wa umma kwenye suala hilo na kwamba kwa sasa wanaanzia shuleni ili kukifanya kizazi hichi ambacho hakijaharibika na mambo hayo kiweze kujua maana na umuhimu wa kuwa na maadili.


     BAADHI YA WALIMU KUTOKA KIGOMA UJIJI WAWAKISIKILIZA MAFUNZO HAYO

 
Baadhi ya walimu waliohudhuria mafunzo hayo akiwemo Mwalimu wa taaluma shule ya Sekondari Kigoma Ujiji, Gervas Gendaneza alisema kuwa kuwepo kwa vilabu vya maadili shule ni muhimu kutokana na mmomonyoko mkubwa wa maadili kwa viongozi na watumishi wa umma kwani itawajengea msingi wanafunzi hao kwa Maisha yao.
 
 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS