Kaimu Mkuu wa wilaya Buhigwe Isack Mwakisu (aliyesimama) akizungumza katika hafla ya upandaji miti 700 iliyotolewa na idara ya uhamiaji na kupandwa katika shule ya Sekondari Biharu wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma
Afisa Uhamiaji mkoa Kigoma Novatus Kato akizungumza katika hafla ya upandaji miti kwenye shule ya sekondari Biharu wilaya ya Buhigwe mkoa kigoma ambapo miti 700 ilipandwa kwenye shule hiyo
Na Fadhili Abdallah,Kigoma
Wananchi wanaoishi vijiji vya mpakani na nchi ya Burundi katika wilaya za mkoa Kigoma kuwa walinzi wa mipaka hiyo kwa kuwafichua na kuwabainisha kwa vyombo vya ulinzi na usalama mkoani humo ili kulinda usalama wa nchi.
Mkuu wa wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma,Isack Mwakisu alitoa rai hiyo wilayani Buhigwe wakati wa hafla ya upandaji miti 700 iliyoandaliwa na Idara ya Uhamiaji mkoa Kigoma katika shule ya sekondari Bihalu iliyopo wilayani Buhigwe mpakani mwa Tanzania na Burundi.
Katika hafla hiyo ambapo Kanali Mwakisu alimwakilisha Mkuu wa wilaya Buhigwe alisema kuwa ulinzi wa nchi ni wajibu wa kila mwananchi ikiwemo kuhakikisha watu wote wanaishi kwa kufuata sheria hivyo wananchi hao wanapaswa kufichua na kuwaripo wageni wanaoingia nchini na kuishi kwenye maeneo yao bila kufuata taratibu za kisheria.
Akizungumzia suala la utunzaji na uhifadhi wa mazingira alisema kuwa ni jambo muhimu kwa Maisha ya binadamu wakati wote na kuhimiza wananchi kuyalinda na kuyahifadhi mazingira yanayowazunguka ikiwemo kupata miti na kulinda uoto wa asili ambao kuhairibiwa kwake kunasababisha matatizo mengi ya mabadiliko ya tabia nchi.
Kwa upande wake Afisa uhamiaji mkoa wa Kigoma, Novatus Kato alisema kuwa serikali haikatazi wananchi hao kuishi na kushirikiana na raia wa kigeni bali ikiwemo kuwatumia kwenye shughuli mbalimbali ikiwemo kilimo lakini alionya kuwa wanapaswa kufuata sheria za nchi kwa raia hao wa kigeni kuwa na vibali vya kuishi nchini na kufanya kazi wakitambulika kwenye mamlaka za serikali.
Afisa huyo wa uhamiaji wa mkoa Kigoma akizungumzia suala la upandaji miti shuleni hapo alisema kuwa kunatokana na kutekeleza mpango wa utunzaji na uhifadhi wa mazingira kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na kwamba kupandwa miti shuleni kunatoa somo kubwa kwa wanafunzi hao kuwa mabalozi wa mazingira ambapo miti 700 ilipandwa shuleni hapo.
0 Comments