Na Hamida Ramadhani, Matukio App Dodoma
TANZANIA ni kati ya nchi zenye idadi kubwa ya wagonjwa wa Saratani ya mlango wa kizazi barani Afrika ambapo inakadiriwa kwamba takribani wanawake zaidi ya Milioni 10 wanapata Saratani ya mlango wa kizaz kill Mwaka Barani Afrika huku wanaopoteza maisha ni zaidi ya Milioni 6 kila mwaka.
Takwimu hizo pia zinaonesha Tanzania ni nchi ya Tatu katika Bara la Africa kwa kuwa na wagonjwa wenye maambukizi mapya ya ugonjwa wa saratani ya Mlango wa Kizazi kwa wanawake.
Hayo yameelezwa na Afisa Mpango wa Taifa wa chanjo Lotalis Gadau kutoka Wizara ya Afya wakati akitoa mafunzo kwa waandishi wa habari kuhusu chanjo ya saratani ya mlango wa shingo ya kizazi (HPV) kuelekea maadhimisho ya Wiki ya wiki ya chanjo ambayo itaanza Aprili 22 hadi 28 mwaka huu.
Amesema wagonjwa wengi wa Saratani ya mlango wa kizazi hawapati huduma za ugunduzi wa haraka na matibabu sahihi
"Asilimia 70 ya wagonjwa wamekuwa wakiwasili katika vituo vya kutolea huduma za afya wakiwa hatua ambayo tayari Saratani imekwisha sambaa katika maeneo mengi ya mwili, "Amesema amesema
Na kuongeza" Takwimu kutoka taasisi ya Saratani ya Ocean Road inaonesha kwamba Saratani ya mlango wa kizazi inachangiwa kwa assilimia 36 ya Saratani zote na asilimia 21 huchangia kwa vifo ," Amesema Dkt Gadau
Pamoja na hayo amesema kuwa wagonjwa wengi takribani asilimia sabini wamekuwa wakifika katika Vituo vya Afya wakiwa na hali mbaya na kutoa wito kwa jamii kuhakikisha wanakuwa na utaraibu wakupima Mara kwa mara ili kuwa salama.
Akielezea kuhusu Chanjo ya Saratani ya Mlango wa shingo ya kizazi amesema Chanjo hiyo ni salama na ni dozi ya Mara moja na inatolewa tofauti na awali ilikuwa inatolewa kwa awamu mbili ambapo wanaopatiwa chanjo hiyo ni watoto wakike kuanzia umri wa miaka9 hadi 14.
"Ni muhimu sasa kwa wazazi kuhakikisha wanawahamasiha Watoto wao kujitokeza kupata Chanjo hiyo ya HPV ili kuwalinda na maambukizi ya ugonjwa huo, " Amesema
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Idara ya Kinga,Wizara ya Afya,Dk.Tumaini Haonga amesema kutokana na ugonjwa kuwa na Kinga Serikali imeamua kuna na Mpango wa kutoa Chanjo hiyo kwa Watoto na mabinti ili kupambana na ugonjwa huo.
Amesema kupitia wizara ya afya wanaendelea na juhudi za kuhakikisha wanatoa chanjo hiyo ili kuwakinga watoto na wanawake kwa ujumla.








0 Comments