Header Ads Widget

“ SERIKALI IPO BEGA KWA BEGA NA NINYI WANANCHI WA LUNGUZA ” DC KUBECHA



Na WILLIUM PAUL, LUSHOTO. 


MKUU wa Wilaya ya Lushoto Japhari Kubecha ameungana na wananchi wa kata ya Lunguza katika ukarabati wa barabara za vijiji katika kata hiyo ambapo amesema Serikali ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ipo bega kwa bega na wananchi wa kata ya Lunguza, katika kutatua kero za wananchi wake. 



Wananchii hao waliojikusanya kwa juhudi zao wenyewe wamesema wanamshukuru Mkuu wa wilaya ya Lushoto Japhari Kubecha kwa kuungana nao katika nguvu kazi ya kuboresha barabara za vijiji, pia wamemshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuwapelekea Mkuu wa Wilaya kijana kwani wameona nguvu kazi yake katika kata ya Lunguza na wilaya kwa ujumla.



Kwa Upande wa Mkuu wa Wilaya Kubecha amesema aliwapongeza wananchii wa kata ya  Lunguza kwa umoja wao, kwa kuungana kwao na kuona waungane waweze kuwa chachu ya maendeleo ya kata ya Lunguza, kwani ni kuunga juhudi za Rais Wa Jamhuri Ya Muunguno wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan

 

 Mwisho.. 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI