Header Ads Widget

RAIS DK. MWINYI ASHUKURU DUA ZA HAYATI MZEE MWINYI


          Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk.Hussein Ali Mwinyi.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema familia ya Hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi imefarijika sana tangu alipofariki dunia kwa Dua zilizofanyika katika maeneo mbalimbali kwa ajili ya kumuombea.

Ameshukuru kwa Dua zilizosomwa kumuombea Hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi.Rais Dk.Mwinyi amesema hayo katika kisomo cha Dua ya Arubaini ya Hayati Ali Hassan Mwinyi pamoja iftari iliyofanyika viwanja vya Ikulu Mnazi Mmoja Aprili 7,  2024.

Kwa upande mwingine Rais Dk.Mwinyi amesema leo ni siku ya kipekee asubuhi imefanyika Hitma ya kuombea Hayati Sheikh Abeid Amani Karume na jioni Hayati Ali Hassan Mwinyi.


Dua hiyo imehudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Serikali, Vyombo vya ulinzi na usalama, Dini , Vyama vya Siasa na Wananchi.





Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI