Na Fadhili Abdallah,Kigoma
Mkuu wa mkoa Kigoma Thobias Andengenye amewataka viongozi wa serikali,viongozi wa dini na wananchi wa mkoa Kigoma kumuunga mkono Raisi Samia Suluhu Hassan ili aweze kuongeza kasi Zaidi katika kuleta maendeleo kwa wananchi mkoani humo.
Andengenye alisema hayo katika futari ya mwezi Mtufukufu wa Ramadhani aliyoandaa kwa viongozi wa serikali, viongozi wa dini na wananchi wa mkoa huo akieleza kuwa awamu ya tatu ya Rais Samia Suluhu kazi kubwa imefanyika katika kutekeleza miradi ya maendeleo mkoani humo.
Alisema kuwa hadi sasa kiasi cha shilingi trilioni 11 zimepokelewa mkoani Kigoma kwa kipindi cha miaka mitatu ya Rais Samia ambazo zimetekeleza miradi mbalimbali inayogusa Maisha ya wananchi wa kawaida moja kwa moja ikiwemo miradi ya afya,elimu miundo mbinu, kilimo na uwezeshaji wananchi kiuchumi.
“Serikali ya awamu ya sita ndiyo imewezesha kuufungua mkoa Kigoma na mikoa mingine na nchi Jirani na huo utashi wa dhati ambao umeonyesha na Raisi Samia kwa wananchi wa mkoa Kigoma hivyo ni jambo jema kuendelea kumuunga mkono kwa nguzu ili afanye makubwa Zaidi ya hayo,”Alisema Mkuu huyo wa mkoa.
Akizungumza katika hafla hiyo ya futari Shekhe wa mkoa KigomaAlhaji Hassan Kiburwa alisema kuwa kama viongozi wa dini na wawakilishi wa wananchi wa mkoa Kigoma wana Imani kubwa na kazi kubwa aliyofanya Raisi Samia.
Shekhe Kiburwa alisema kuwa mkoa Kigoma umepiga hatua kubwa kimaendelea kutokana na miradi mikubwa ambayo imetekelezwa na inayoendelea kutekelezwa hivyo wao kama viongozi wa dini watamuombea kiongozi huyo afya njema ili aendelea kufanya kazi hiyo kwa bidi Zaidi.
0 Comments